Serikali yetu ama kwa kujua au kwa kutokujua au kwa kushauriwa vibaya, iliwafukuza wauguzi wazoef na waliobobea na wenye ujuzi na wito na kazi ya uuguzi kwa vigezo vya kutokuwa na vyeti. Sasa wamebaki na wenye vyeti ambao wanawakimbia wagonjwa. Tusiwe tunafanya maamuzi kwa kukurupuka bila kuangalia madhara yake jamani. Na sis wananchi tuliokuwa tunashangilia wale manes Mama zetu wakilia kwa kufukuzwa kazi sasa hiv ndio tunalia kwa kukimbiwa na wahudum na madaktari.
Sio mahospitalini tu wanapata tabu ya kuondoa watu wazoef, hata sehem nyingine mfano bandarini Tpa wiki iliyopita kuna gari ilitumbukia baharini ikiwa na wafanyakazi wanne sem yenye kina cha mji kama mita 14. gari ilikuja kutolewa wameshafariki wote. Lakini kama wale madiver wazoef waliofukuzwa kwa kutokuwa na vyeti wangekuwepo wangezamia na kuokoa wale watu na wasingekufa. Tunao madiver kweli waajiwa wapya na wenye vyeti vizuri lakin uzoef hawana.
Sem nyingi kuna shida ukienda upande wa madereva wote ni mashahd tunaona yanayofanyika barabarani.
Sent using
Jamii Forums mobile app