Ummy Mwalimu: Watoa huduma za afya wasikimbie wagonjwa, sio kila homa kali ni Corona

Tena bahati mbaya sio hawana vyeti kabisa,walikuwa navyo vya uuguzi ila tu eti cheti cha form four?!!

Yaani mtu anafanya kazi vizuri tena unakuta ndio anajitoa na kuokoa maisha ya wagonjwa,halafu unamwambia hana cheti cha form four?!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
hiko sio kigezo, huwezi ukaambiwa uhudumie mgonjwa wa corona huku huna vifaa vya kujikinga na wewe ukajitoa kimaso maso eti uzalendo, huo ni uwendawazimu.
Hiyo ndiyo sababu kubwa,,, upo sahihi boss
Vifaa vya kujikinga ni tatizo.


Tuendelee kupiga goti.[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inamaana kabla ya maambukizi ya corona vitro vya afya havikuwa na maji tiririka kwa wahudumu kunawa mikono?
 
Kuna kitu kinafichwa hapa lakini muda ni mwalimu mzuri. Waswahili wanasema huwezi kuficha kaa la moto mfukoni
 
Haya sasa mapya.

Mgonjwa anakimbiwa na watoa huduma wa sekta ya Afya!

Nani wa kumuangalia Mgonjwa?

Nani wa kuokoa Maisha ya Mgonjwa?

Siwalaumu sana, labda hawana vifaa vya kutosha vya kujikinga.

Sikatai, unaweza ukawa na vifaa vya kutosha vya kujikinga, na bado mtoa huduma wa sekta ya Afya ukaambukizwa.

Haya mambo yanataka Moyo.

Wenzetu tunaowaona wenye shughuli zao nyingine, na wanajitolea kufanya kazi hizi kipindi hiki kigumu, mfano unakuta ni Mwanamichezo.

Mwanamichezo, na sekta ya Afya siyo shughuli zake, lakini mtu anajitolea kufa na kupona kuokoa Maisha ya watu wengine.

Kwa kweli wanastahili pongezi ya hali ya juu
 
Uuguzi Ni wito,,hii ya wauguzi kukimbia wagonjwa ndo nimesikia mwaka huu,haijawahi kutokea popote
Ni wito lakini wanatakiwa kupewa vitendea kazi. Hakuna hata goggles unavaa barakoa na kunawa mikono, mgonjwa akikukoholea usoni umekwisha.
 
Waziri wa afya mh Ummy Mwalimu amewataka wahudumu wa afya katika hospitali za serikali na binafsi kutowakimbia wagonjwa wa Corona.

Kadhalika waziri Ummy ametoa wito wagonjwa wa Corona na wale waliopona wasinyanyapaliwe kwa namna yoyote ile.

Source: Mtanzania
 
Waende kavu kavu kwa covid 19 patients?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…