Mkuu asante kwa maelezo, ningependa kujua zaidi kuhusu UTT, lakini kabla sijaenda ofisini kwao nasoma website yao naona aina tofauti nini kinasababisha bei kuwa tofauti? Idadi ya watu kwa kila fungu au? Na unaposema kwa hela ndogo ununue vipande sio hisa, kwenye web yao sioni hilo neno, vipande ndio 'chips?' na je nitawaambiaje wakati nanunua kuwa sio hisa au watatoa maelezo zaidi. Uelewa wangu kuhusu hisa ni mdogo na info nyingi zimekuwa na negativity kiasi sikuweza kufatilia kabisa.
Mkuu, UTT wana aina tofauti tofauti za mifuko kwa ajili ya madhumuni tofauti na si kwa sababu ya idadi ya watu. Kwa mfano, ukitaka kuwekeza kwa ajili ya kumlipia mtoto wako gharama za masomo basi itabidi uingie mfuko wa watoto na ukitaka kukuza mtaji wako itabidi uingie mfuko wa umoja. Upo ambao ni kwa ajili ya wastaafu wanaopata gawio japo hata asiyekuwa mstaafu anaruhusiwa kuwekeza pia kwenye mfuko huo na nadhani unaitwa jikimu. Neno vipande ni kama hizo hizo hisa na ndo linalotumika kumaanisha hisa kwa UTT. Wewe unanunua vipande (units) kwao UTT na wao wanatumia hiyo pesa yako pamoja na za wengine waliowekeza kwenda kununua hisa kwenye makampuni tofauti tofauti. Rejea mchango wangu namba 10 hapo juu kwenye uzi huu nilipokuwa namjibu hopaje.