Umoja wa Machifu mkoa wa Mara watoa ONYO kwa wanasiasa wanaotoa matamshi ya kutotambua umuhimu wa Machifu nchini

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Umoja wa Machifu Mara umekutana na vyombo vya habari nakutoa Onyo kwa baadhi ya Wanasiasa wanaotoa matamshi ya kuonesha kutotambua umuhimu wa Machifu nchini na kuwasihi watanzania wawaone Wanasiasa hao kama watu wenye nia ya kuvunja umoja wa kitaifa.

Pia soma > Humphrey Polepole: Mambo ya machifu hayana msaada kwa taifa, yanaweza kuleta ukabila na mgawanyiko, yanapaswa kupingwa

Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Mara, Japhet Wanzagi amesema kuwa kama mnavyojua Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mkuu wa Machifu wote nchini kwa jina la Chifu Hangaya sisi kama Machifu wa mkoa wa Mara tumejipanga kumpokea Chifu wetu.

Kuna mtu alikuwa anasema Machifu hawakuwepo, machifu walikuwepo muda mrefu tangu kipindi cha mkoloni. Mtu anayesema Machifu walipandikizwa na mkoloni na wakaondolewa na Baba wa Taifa huyo ni muongo.

Machifu walitolewa kwenye mamlaka ya Serikali lakini walirudi kuwa viongozi kwenye jamii zao, ila katika kipindi cha awamu ya Sita, Rais Samia ametupa heshima sana Machifu.

Majukumu yetu makubwa sisi Machifu ni upatanishi hasa kuanzia ngazinya familia mpaka ngazi ya mamlaka za juu na mara nyingi uwepo wetu umesaidia kutatua migogoro kwenye jamii zetu.

Naye Dkt. petter Makomara ambaye ni msemaji wa kabila la Wasorwa amesema kuwa

Sisi Machifu wa Mara tunamuahidi Chifu wetu Hangaya ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa tutaendelea kulinda amani yetu ili kupunguza matukio ya kiuhalifu kwa Mara.

Kuna rasimu inashughulikiwa ipo Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo itatuhusisha sisi Machifu hasa kwenye migogoro na mwisho wa siku tutapunguza baadhi ya matukio ya jinai.

Chifu wa Kiseru Rorya, Msangia Ngoje yeye amedai kuwa kuna watu wanaandika mtandaoni na kutukosea heshima Machifu, wengine tunawafahamu wana laana kweye koo zao huko nyumbani, ndio maana kila siku wanaongelea Dar es Salaam mara Morogoro au mtandaoni na nyumbani kwao hawaendi.

Tunashauri inapotokea matukio ya kijinai viongozi wa kiusalama wa mkoa waje kutufuata Machifu ili tuweze kukemea na kuondoa laana kwenye hizo koo.

Ma1.jpg
ma2.jpg

Mwisho.
 
Aisee!!
 
Suala la kuukuza uchifu TZ linaturudisha nyuma.Hayati J.K. Nyerere aliona mbali.Kama serikali ya ccm inaona halina madhara basi himizeni kila kabila lifufue uongozi wa kichifu.
 
Back
Top Bottom