Umoja wa Madereva wa Mtandaoni (UMM) wamshukuru Rais Samia kwa Mazingira Wezeshi

Umoja wa Madereva wa Mtandaoni (UMM) wamshukuru Rais Samia kwa Mazingira Wezeshi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
▪️ _Umoja wa Madereva wa Mtandaoni (UMM) wamshukuru Rais Samia kwa Mazingira Wezeshi, Wawataka Watanzania Watumie SwifPack

UMM umeendelea “kukiwasha hadi SABASABA” baada ya kufanya matembezi ya hiari leo tarehe 28 Juni 2025, katika viwanja vya Maonesho ya SABASABA jijini Dar es Salaam, wakitangaza kwa nguvu huduma mpya ya usafiri wa mtandaoni ya SwifPack inayotolewa na Shirika la Posta Tanzania.

Maandamano haya yameambatana na wito kwa Watanzania kuichagua SwifPack kama njia Salama, Nafuu, na ya Kisasa ya usafiri kuelekea na kutoka kwenye Maonesho ya SABASABA 2025. SwifPack, ambayo ilizinduliwa rasmi Januari 2025, imepokelewa kwa hamasa kubwa na madereva wa mtandaoni kutokana na mfumo wake wenye uwazi, makato nafuu na fursa pana ya kiuchumi.

Mwenyekiti wa UMM, Bw. Issa Swahibu, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora ya biashara na teknolojia, yaliyowezesha ujio wa huduma hii ya ubunifu. “SwifPack si tu App ya usafiri, bali ni jukwaa la kuwakomboa madereva wa Kitanzania,” alisema Bw. Swahibu.

Kwa sasa, madereva wa SwifPack wameahidi kuendelea kuhamasisha matumizi ya huduma hii hususani katika msimu huu wa Maonesho ya SABASABA, kwa kuwaamini Watanzania watapokea kwa moyo mabadiliko yanayolenga Usalama, Urahisi na Ujumuishaji wa kijamii kupitia teknolojia ya Posta.
IMG-20250629-WA0004.jpg
IMG-20250629-WA0011.jpg
IMG-20250629-WA0014.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250629-WA0005.jpg
    IMG-20250629-WA0005.jpg
    166.1 KB · Views: 36
  • IMG-20250629-WA0012.jpg
    IMG-20250629-WA0012.jpg
    985.6 KB · Views: 34
  • IMG-20250629-WA0017.jpg
    IMG-20250629-WA0017.jpg
    883.3 KB · Views: 31
  • IMG-20250629-WA0006.jpg
    IMG-20250629-WA0006.jpg
    128.7 KB · Views: 29
  • IMG-20250629-WA0008.jpg
    IMG-20250629-WA0008.jpg
    793.4 KB · Views: 26
  • IMG-20250629-WA0016.jpg
    IMG-20250629-WA0016.jpg
    838.5 KB · Views: 33
Hii inahusiana na safari za ungo? Sijaelewa kwani sioni magari naona madereva na mabango.
 
Back
Top Bottom