PostGE2025 Umoja wa Mataifa (UN) watoa wito kwa Serikali ya Tanzania kulinda waandamanaji wa 9 Desemba, 2025

PostGE2025 Umoja wa Mataifa (UN) watoa wito kwa Serikali ya Tanzania kulinda waandamanaji wa 9 Desemba, 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
GENEVA - Disemba 05, 2025

Serikali ya Tanzania imehimizwa kudumisha uhuru wa kimsingi kabla ya maandamano yaliyopangwa ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Disemba.

Msemaji wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu amezikumbusha mamlaka juu ya wajibu wao wa kulinda haki za uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa amani na kujumuika. Ametoa wito kwa vikosi vya usalama kupanga na kutekeleza operesheni kwa njia zinazoruhusu raia kutekeleza haki hizi kikamilifu.

Wito huo unajiri huku kukiwa na ripoti kwamba mamia ya watu waliuawa na zaidi ya 2,000 kushikiliwa kufuatia maandamano ya baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, baada ya hapo mamlaka ilizidisha msako dhidi ya wapinzani ambao ulifikia kilele cha kupiga marufuku maandamano nchini kote yaliyotangazwa tarehe 3 Disemba.

Chini ya sheria ya kimataifa, Magango alibainisha, silaha za moto kamwe zisitumike kutawanya maandamano na zinaweza tu kutumiwa kama suluhu la mwisho kukabiliana na vitisho vya kifo au majeraha mabaya.

Umoja wa Mataifa ulikariri kuwa makamanda wa vikosi vya usalama wana wajibu wa kuhakikisha kwamba kanuni hizi zinaheshimiwa kabla ya maandamano yoyote, ikisisitiza kwamba Siku ya Uhuru wa Tanzania inapaswa kuadhimishwa kwa uhuru, na sio ukandamizaji.

====

The UN human rights office on Friday called on Tanzanian authorities to ensure fundamental freedoms are respected ahead of planned demonstrations on the country's Independence Day, urging security forces to allow peaceful assemblies amid escalating tensions following last month's elections.

Ahead of planned Dec. 9 protests, "we remind the authorities of their obligation to ensure the rights to freedoms of expression, peaceful assembly, and association," spokesperson Seif Magango told reporters in Geneva.

"We urge the government to instruct security forces to plan and implement their operations in a manner that allows Tanzanians to fully exercise these fundamental rights," he added.

Magango said hundreds were reportedly killed and over 2,000 detained after protests erupted following the Oct. 29 general elections, adding that the government had "intensified a crackdown against opponents since the vote."

He noted that a nationwide police ban on all Independence Day protests issued on Wednesday constituted "an overbroad, disproportionate step," calling for the lifting of the ban.

"We remind security forces they must refrain from using force to disperse non-violent assemblies and make every effort to de-escalate tensions," he said. "We recall again the requirements of international law in this area -- if unavoidable, any use of force, including less lethal weapons, must be restricted to the minimum extent necessary. Firearms should not be used to disperse any assembly and can only be used as a measure of last resort to counter an imminent threat of death or serious injury."

Magango warned that recent detentions of academics, civil society actors and political figures, some allegedly carried out by unidentified armed personnel, alongside increased security deployments, fuel restrictions and expanded digital surveillance "risk inflaming public tension."

He stressed that authorities have yet to disclose how many people were killed in the post-election unrest or clarify reports of enforced disappearances.

"The continued absence of transparent information risks further eroding public trust and heightening tensions at a critical moment," he said, calling for the "immediate and unconditional release" of all those arbitrarily detained.

Magango noted the government has launched an investigation into the violence. He said UN human rights chief Volker Turk reminded authorities that such a probe must meet international standards of independence, impartiality, thoroughness, promptness and transparency, and ensure protection from reprisals for all who engage with it.

Source: AA
 
Screenshot_20251121-231231_1.jpg
 
Muwe mnaweka na source
Hivyo ndio umahari wa kuleta habari kwa jamii , sio mnalopoka tu kama mtoa taarifa


 
Policcm jukumu lao sio kuzuia maandamano bali kulinda waandamanaji hawakufanya jukumu hilo October 29 wakaua waandamanaji na wasio waandamanaji na ushahidi wa picha na video upo wazi.

Sheria inataka waandamanaji watoe taarifa tu ambacho wamekifanya na inajulikana maandamano yao wameyaita D9 , policcm wako busy kuzunguka kudai wamezuia maandamano.
 
Muwe mnaweka na source
Hivyo ndio umahari wa kuleta habari kwa jamii , sio mnalopoka tu kama mtoa taarifa


 
Dunia ina mambo ya ajabu sana tuliokua tunamuimba Kaburu kila kukicha kwenye mchakamchaka sasa hali ya Makaburu wapo home Tanzania sio daah inaumiza sana kila nikifungua radio za huku NJ Tanzania Tanzania aisee..
 
Kwaiyo vijana wa GN Z waachwe waandamane maandamano yasiyo na kikomo yenye Lengo la kuipindua serikali!!
Ata wewe Afisa wa UN ungekuja kushiriki na utambulisho wako wa UN Bado ungepigwa chuma hadharani.
Hakuna Dola inaweza kuchezewa kwa kiwango icho.
 
GENEVA

Serikali ya Tanzania imehimizwa kudumisha uhuru wa kimsingi kabla ya maandamano yaliyopangwa ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Disemba.

Msemaji Seif Magango wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu alizikumbusha mamlaka juu ya wajibu wao wa kulinda haki za uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa amani na kujumuika.

Alitoa wito kwa vikosi vya usalama kupanga na kutekeleza operesheni kwa njia zinazoruhusu raia kutekeleza haki hizi kikamilifu.

Wito huo unajiri huku kukiwa na ripoti kwamba mamia ya watu waliuawa na zaidi ya 2,000 kuzuiliwa kufuatia maandamano ya baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, baada ya hapo mamlaka ilizidisha msako dhidi ya wapinzani ambao ulifikia kilele cha kupiga marufuku maandamano nchini kote yaliyotangazwa tarehe 3 Disemba.

Chini ya sheria ya kimataifa, Magango alibainisha, silaha za moto kamwe zisitumike kutawanya maandamano na zinaweza tu kutumiwa kama suluhu la mwisho kukabiliana na vitisho vya kifo au majeraha mabaya.

Umoja wa Mataifa ulikariri kuwa makamanda wa vikosi vya usalama wana wajibu wa kuhakikisha kwamba kanuni hizi zinaheshimiwa kabla ya maandamano yoyote, ikisisitiza kwamba Siku ya Uhuru wa Tanzania inapaswa kuadhimishwa kwa uhuru, na sio ukandamizaji.

wavimba_20251205_175447_0000.png

Amani ndio nguzo ya maendeleo ya Tanzania , bila utulivu hatuwezi kujenga uchumi imara, elimu bora, afya na fursa sawa kwa wote. Uhuru tuliopewa ni wajibu wa kuendeleza misingi ya waasisi wetu kwa kuungana, kushikamana na kulinda maadili ya taifa. Tunapoadhimisha siku ya uhuru, tuitumie kama nafasi ya kuombea Tanzania yetu, kuimarisha umoja na kuendeleza uzalendo unaotujenga kuwa nguvu moja dhidi ya changamoto za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Maombi, mshikamano na upendo kwa taifa letu ndizo baraka na kinga ya Tanzania tunayoitamani. #uhuru #tanzania #africa #independence #december
 
Kwa bahati mbaya, hawa wooote ni watu wa kuuza maneno tuuu; hawana msaada muhimu kwa mahitaji yetu.

Kazi hii ni yetu waTanzania kuifanya. Hatuwezi kutegemea maneno matupu kuleta mabadiliko .
Mkuu,
Hawa wakiingia ni last resort, wakiingia wanamng'oa aliyeko madarakani. Usipuuze wanayoongea hata kidogo. Wanatumia diplomasia vizuri tu, wakiona huelewi wanaingia na kumalizana na wewe.
 
Back
Top Bottom