Umoja wa Mataifa: Watu milioni sita wahitaji misaada Ethiopia

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na dharura inasema zaidi ya watu milioni sita katika maeneo kame ya mashariki na kusini mwa Ethiopia watahitaji msaada wa kuyaokoa maisha yao mwaka huu.

Shirika hilo linasema zaidi ya watu milioni 6.4 katika maeneo yaliyoathirika wanakadiriwa kuhitaji msaada wa chakula mwaka huu na wakati ambapo serikali ya Ethiopia na washirika wake wa misaada ya kiutu wakiwa wanashirikiana kukabiliana na mgogoro huo, mahitaji ni makubwa mno kuliko misaada iliyoko.

Ukame unaifanya hali ya kiutu kuwa mbaya zaidi nchini Ethiopia ambako vita kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa TPLF kaskazini mwa nchi hiyo vimewaacha mamilioni ya watu wakihitaji misaada.

Karibu watu milioni tatu katika maeneo ya Somali na Oromia Kusini wanakabiliwa na matatizo ya maji huku idadi nyengine ya watu isiyojulikana wakiwa wamelazimika kuyakimbia makaazi yao.
 
waache wapigane vita, sisi tutawauzia mahindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…