Umoja wa ulaya (EU) waidhinisha Bilioni 461 kwa Tanzania

Umoja wa ulaya (EU) waidhinisha Bilioni 461 kwa Tanzania

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Umoja wa Ulaya (EU) umerudisha rasmi upatikanaji wa fedha za maendeleo za kiasi cha Euro milioni 156 (takribani Shilingi bilioni 461 za Tanzania) baada ya kuchelewesha kuidhinishwa kwa mpango huo baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya EU nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki Ndg Marc Stalmans, uamuzi huo ulifanywa Julai 23, 2026 kwamba EU itaendelea na utoaji wa kiasi chote cha fedha hizo bila kupunguza bajeti wala kubadili upeo wa malengo ya shughuli zilizopangwa awali.

Umoja wa Ulaya mbali na kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania pia ni kinara wa ushirikiano wa maendeleo ya sekta za kilimo, nishati, miundombinu, biashara na teknolojia. Takwimu za EU zinaonesha biashara baina ya pande hizi mbili ni Euro Bilioni 2.15 kwa mwaka 2025.
 
Back
Top Bottom