Tumain
Ni umoja gani wa upinzani unaosema, wa vyama vya siasa wa viongozi au wa wananchi?
Kama ni wa vyama, vyama vyenyewe CUF+Chadema+TLP+UDP+NCCR+... kifupi hautakuwepo i dont see light at the end of the tunnel, opposition alliance is like a dream especially in Tanzania, Lengo la umoja nikusaidiana lakini kama unaona mwenzako hakusaidii anakusaliti umoja hauna haja tena na hakuna mtu atakayekulaumu, mfano wakati wa uchaguzi mdogo Tarime vyama tulivyokuwa tunategemea visaidiane ndivyo vikawa mpinzani mkuu wa CHADEMA kuliko hata CCM wenyewe.
Umoja hautakuwepo kwa sababu kila chama kina ideology yake malengo yake madhumuni yake na sera zake. Chadema kina sera ya majimbo sijui kama CUF wana sera hiyo hata kama wakiwa na sera hiyo watatofautiana wakati wa kuiuza kwa wananchi. Afterall viliwahi kuunda umoja ukaitwa UDETA matokeo yake ukaingiliwa na virus ukafa lilikuwa ni somo tosha kwa upinzani.
Kama unasema umoja wa Viongozi, viongozi wenyewe ni Lipumba+Mbowe+Mrema+Cheyo+Mbatia+Mtikila+... nawaheshimu sana hawa viongozi kwa sababu si kila mtu anaweza kujitolea na kuwa mstari wa mbele kutetea masilahi ya Taifa tusiwalaumu, ukimulaumu Lipumba au Mbowe utakuwa hujawatendea haki jaribu wewe kuwa mwenyekiti uone. Ingawa lengo lao ni moja lakini kila kiongozi niliowataja ana maslahi yake, wengine wako kweli kwa maslahi ya wananchi lakini wengine wako kwa maslahi binafsi hiyo ni hulka ya binadamu.
Kwa mawazo yangu kwavile kila mmoja anajali maslahi yake sidhani kama watakuja kuwa kwenye chungu samahani chama kimoja. Kila mtu atataka awe ndiye na sauti kuu (boss) nani atakubali? hebu niambie wakiungana Mtikila atataka awe msemaji mkuu Cheyo mtunza fedha Mbatia naye atazitaka mwisho ni kushikana mashati kugombea uenyekiti kama yaliyotokea kati ya Mrema na Marando wakati wa NCCR kule Raskazone Tanga. Kwa hiyo ni vigumu sana kwa viongozi wetu tulionao kuungana unahitajika ukomavu hasa wa akili kisiasa si lazima uwe wa darasani hekima na busara kubwa.
Kama unasema Umoja wa wananchi, kwa mawazo yangu nafikiri unawezekana, unawezekana kwa misingi ifuatayo; Ni rahisi kuwaunganisha wananchi wa kawaida (wanachama) kuliko kuwaunganisha viongozi. Lengo kuu la wananchi 'ninaposema wananchi namaanisha wanachama vilevile' si muungano wa vyama ni kuwa na maendeleo kwenye jamii zao kwenye familia zao. Wanataka kiongozi au chama kimoja chenye kuwapa matumaini iwe kwa vitendo au hata kwa ahadi. Chama kimoja chenye nguvu na itikadi moja chama kinachoonekana kuwajali kuwasikiliza na kuwa karibu nao ni kama mtoto anavyopenda. Chama kitakachowasemea kiwe kama kipaza sauti chao pindi wanapokuwa na tatizo wapweke. Kwa sasa wanajiona kama wapweke chama walichokuwa wanakitegemea CCM hakiwajali tena kimewasahau. Hawahitaji muungano wanahitaji chama chenye nguvu hata kikiwa pekee.
Nirahisi kuwaunganisha na kuwaongoza wananchi wa kawaida milioni 5 kuliko kuwaunganisha viongozi wawili au vyama viwili.