Moja ya madai Yao ni kwa nini kuna watu waliomaliza nao waneajiriwa bila kufanyiwa usaili?Ila waalimu bhana, yn wanataka ulinzi kutoka kwa mtu huyo huyo wanayemuhitaji 😂 labla wangesema wanakwenda na ulinzi wao wenyewe.
Sasa mtu umefeli usaili afu unataka ulinzi, nani amdhuru mtu anayepata 0% kwenye usaili 😂
Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO) umetangaza kuwa uko tayari kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa ajili ya majadiliano kuhusu ajira za walimu nchini. Hata hivyo, NETO imesisitiza umuhimu wa kuhakikisha usalama wa viongozi wake kufuatia vitisho wanavyodai kupokea kupitia simu na jumbe mbalimbali.
Chama ca Walimu Wasio na Ajira (NETO) kimesema kimepokea wito wa Waziri George Simbachawene wa kufanya mazungumzo kuhusu usaili wa walimu uliofanyika kati ya Januari 14 na Februari 24, 2025, lakini kimeomba kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha kwa washiriki wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa NETO, Daniel Edigar Mkinga, amesema lengo lao ni kushinikiza serikali kutoa ajira kwa walimu wasio na kazi na kufanyia kazi mapendekezo yao. Pia, NETO imeomba mazungumzo hayo yahusishe viongozi wa dini na wawakilishi wa mikoa mbalimbali ili kuhakikisha yanafanyika kwa uwazi na amani.
“Lakini kutokana na vitisho tunavyopokea kwenye simu na jumbe mbalimbali zinazozidi kutupa hofu juu ya usalama wetu, tunaomba kuhakikishiwa ulinzi na usalama wetu katika mkutano huo”, imeelezwa katika barua hiyo.
Mara baada ya mkutano huo, viongozi wa NETO wanatarajia kwenda kuwaeleza walimu wenzao kuhusu maazimio ya mazungumzo hayo, wakibeba matumaini mapya kwa mustakabali wa ajira zao.
Sasa mambo ya kuajiriwa bila usaili yameshapita, sasa hv lazima usaili.Moja ya madai Yao ni kwa nini kuna watu waliomaliza nao waneajiriwa bila kufanyiwa usaili?
Wanammudu Simbachawene ndio maanaHuu ni utoto
Ila waalimu bhana, yn wanataka ulinzi kutoka kwa mtu huyo huyo wanayemuhitaji 😂 labla wangesema wanakwenda na ulinzi wao wenyewe.
Sasa mtu umefeli usaili afu unataka ulinzi, nani amdhuru mtu anayepata 0% kwenye usaili 😂
Ohoo!Tayari Kimeshaumana......
Waliopata 0 wametoka wapi, yn kila siku pdf zinatoka na 0 afu unakuja kubisha hapa ww vpunajikutaga special, kuna m2 wa kupata zero mitihani ya utumishi?? tena ualimu
kwahiyo nawew kwa akili zako kabisa zile unaamini ni zero halisi???Waliopata 0 wametoka wapi, yn kila siku pdf zinatoka na 0 afu unakuja kubisha hapa ww vp
Ni za kutengeneza.kwahiyo nawew kwa akili zako kabisa zile unaamini ni zero halisi???
Utoke Scotland yard.Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO) umetangaza kuwa uko tayari kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa ajili ya majadiliano kuhusu ajira za walimu nchini. Hata hivyo, NETO imesisitiza umuhimu wa kuhakikisha usalama wa viongozi wake kufuatia vitisho wanavyodai kupokea kupitia simu na jumbe mbalimbali.
Chama ca Walimu Wasio na Ajira (NETO) kimesema kimepokea wito wa Waziri George Simbachawene wa kufanya mazungumzo kuhusu usaili wa walimu uliofanyika kati ya Januari 14 na Februari 24, 2025, lakini kimeomba kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha kwa washiriki wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa NETO, Daniel Edigar Mkinga, amesema lengo lao ni kushinikiza serikali kutoa ajira kwa walimu wasio na kazi na kufanyia kazi mapendekezo yao. Pia, NETO imeomba mazungumzo hayo yahusishe viongozi wa dini na wawakilishi wa mikoa mbalimbali ili kuhakikisha yanafanyika kwa uwazi na amani.
“Lakini kutokana na vitisho tunavyopokea kwenye simu na jumbe mbalimbali zinazozidi kutupa hofu juu ya usalama wetu, tunaomba kuhakikishiwa ulinzi na usalama wetu katika mkutano huo”, imeelezwa katika barua hiyo.
Mara baada ya mkutano huo, viongozi wa NETO wanatarajia kwenda kuwaeleza walimu wenzao kuhusu maazimio ya mazungumzo hayo, wakibeba matumaini mapya kwa mustakabali wa ajira zao.
Jiulize tu swali rahisi, hivi kwenye hixo multiple choices questions za utumishi hakuna miamba inyopiga 100 mbona hatuzioni, ndo utapata uhalisia wa hizo zero.Ni za kutengeneza.
Una uhakika maswali yalikuwa n multiple choices?Jiulize tu swali rahisi, hivi kwenye hixo multiple choices questions za utumishi hakuna miamba inyopiga 100 mbona hatuzioni, ndo utapata uhalisia wa hizo zero.
Ujinga wa watawala wa CCM ni kama watakuwa na mawazo kama yako..Wanaenda kupotea tu, Kundi lenyewe litaonekana halina usajili rasmi ni la mtandaoni. Utasikia tu wakibanwa nani amewatuma . Wanataka kusikia ni chadema wamewatuma. Subiri mje msikie
Naona mabadiliko yapo njiani, vijana sasa hawaogopi. Tulizungumza tangu zamani kwamba ukosefu wa ajira wa makusudi unaosababishwa na serikali ni bomu linalosubiri kulipuka muda wowote. Vyama vya upinzani sasa vije na hoja nzuri mezani vijana wapo tayari maana wanauelewa wa kutosha wa masuala ya maisha, hawana utoto tena ground kwa moto.
Kwa wauza ubongo wa kijani?wakishasajiliwa tu wanaporo ubongo wakiaminishwa hawata uhitaji tena.Rejea wanaojiita chawa wao?Ujinga wa watawala wa CCM ni kama watakuwa na mawazo kama yako..
Tatizo sio walimu hao. Tatizo ni mfumo mibaya iliyosababishwa na sera mbovu za kiuchumi za CCM. Waambieni wenye maamuzi washughulikieni hilo....!!
Kutisha wakosoaji wa sera na mipango mibovu ya serikali sio suluhu na haitaondoa tatizo....
Suluhu ni kusikiliza hoja na kuzipima ktk ukweli wake na kisha kuchukua hatua sahihi za kiutawala na maamuzi...
Serikali iache mara moja kutisha watu badala ya isikilize watu na kushughulikia matatizo yao na kama ni lazima na ni muhimu, basi mifumo ya utendaji, kisheria na kisera irekebishwe...