Umri gani sahihi mtoto kuingia chekechea!!

BABA E's

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
354
Reaction score
135
Habari za Jumamosi wanaJF. Nina mtoto ambaye anakaribia miaka mitatu. Tupo kwenye mabishano kidogo na wife kwamba mtoto aingie chekechea au la!. Mama anasema umri huo unatosha, lakini mimi naona mtoto bado, labda mwakani. Nikimwangalia mtoto naona bado anahitaji kuwa karibu zaidi na wazazi kuliko huko shule. Kuna baadhi ya shule tumejaribu kutembelea huko tumekuta watoto wadogo zaidi ya mtoto wetu, lakini nimeshindwa kupata jibu kamili hasa kwanini wazazi wanapeleka watoto wakiwa wadogo kiasi hicho. Watoto wenyewe wengi walikuwa wanalia tu mda wote wanaita mama, sasa mimi kwa upande wangu nahisi haya ni kama mateso kwa mtoto, lakini mama anasema ni bora aende sasa ili ajifunze kukaa na watoto wenzake. Nyumbani tunapokaa watoto si wengi. Enzi zetu wengi tulikuwa tunaingia tukiwa na miaka mitano, ingawa wapo walioingia chini ya hapo kwa sababu maalum hasa kama shule ipo karibu sana na nyumbani. Shule tunayoweza kumpeleka ipo mbali kidogo na nyumbani kwahiyo kuna magari ambayo yatakuwa yanapitia watoto asubuhi saa moja na kuwarudisha saa tisa mchana. ndugu zanguni mliopitia kwenye haya hebu tupeni ushauri.
 
naongea kama mzazi na si kama mtaalamu wa mambo ya elimu, miaka mitatu inatosha kabisa kuanza chekechea, mpe wiki moja tu utakuta anakufundisha mavitu aliyofundishwa shule hata kuimba tu (labda awe nunda), ila tatizo linawezakuwa kwenye kuamka asub, ila unaweza kuanza na shule za mchana anaingia school saa 5 na kurudi saa 9 mchana, the opposite subiri mpaka atakapo kusimulia nani alilala na house girl/boy wenu chumbani kwenu wakati mkiwa kazini
 

Nashukuru kwa ushauri, Tatizo kwangu litakuwa ni umbali wa shule. Na hizo gari za shule ni asubuhi wakati wa kwenda na mchana saaa tisa wakati wa kurudi.
 
Nashukuru kwa ushauri, Tatizo kwangu litakuwa ni umbali wa shule. Na hizo gari za shule ni asubuhi wakati wa kwenda na mchana saaa tisa wakati wa kurudi.
Sikushauri kumpeleka shule, kwa kweli kumpandisha gari asubuhi mtoto wa umri huo na kumrudisha saa tisa ni mateso. Najua wapo watakaopinga kwa kuwa wamefanya hivyo, lakini kama wao wamewatesa watoto wao si lazima kila mtu afanye hivyo. Alternatively, mnaweza mkawa mnamfundisha hapo hapo home hata kama kwa saa moja kwa siku, atajua baadhi ya vitu na hautakuwa na hofu ya kuwa mbali na mtoto. Akifikisha miaka minne mtafutie shule ya karibu, hata kama ni tuisheni ya kuzugia ya mtu binafsi. Miaka mitano mpeleke pre-unit, miaka sita darasa la kwanza. Siwezi kumtesa mtoto wangu mimi!
 
unaweza kufuata ushauri #4 hapo juu utafute shule ya karibu ili kumaliza issue ya usafiri, lakini kikubwa ni ubora wa shule, kama ipo mbali hauna namna inabidi aamke mapema, ila tukirudi kwenye hoja ya msingi - umri wa miaka 3 inawezekana kabisa mtoto kuanza shule, ni time nzuri kwa mtoto kuanza kujichanganya na wenzake
Nashukuru kwa ushauri, Tatizo kwangu litakuwa ni umbali wa shule. Na hizo gari za shule ni asubuhi wakati wa kwenda na mchana saaa tisa wakati wa kurudi.
 

Nashukuru sana kwa ushauri. hapo ndipo kichwa kinapouma.
 
mtoto kisha jua kuongea tu, mpeleke chekechea mkuu.
 
Mimi wangu alikuwa wa umri huo alikuwa anasumbua sana....mama nataka kwenda shule,akiamka tu ndio ulikuwa wimbo.
Nikampeleka shule akiwa na miaka 3 na miez9....week ya kwanza ilipoisha akaja style nyingine.Mama sipendi shule....! Alikuja kuzoea lakini.
Angalizo: Miaka4 kwenda mitano ni muda sahihi kwa mtazamo wangu! Ila nyumbani apate shule kama walivyosema wachangiaji wengine hapo juu.
 
mitatu ndio mizuri ili mitano la kwanza ndio miaka mizuri hio..
 
Aende..if possible pata skuli ya karibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…