BABA E's
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 354
- 135
Habari za Jumamosi wanaJF. Nina mtoto ambaye anakaribia miaka mitatu. Tupo kwenye mabishano kidogo na wife kwamba mtoto aingie chekechea au la!. Mama anasema umri huo unatosha, lakini mimi naona mtoto bado, labda mwakani. Nikimwangalia mtoto naona bado anahitaji kuwa karibu zaidi na wazazi kuliko huko shule. Kuna baadhi ya shule tumejaribu kutembelea huko tumekuta watoto wadogo zaidi ya mtoto wetu, lakini nimeshindwa kupata jibu kamili hasa kwanini wazazi wanapeleka watoto wakiwa wadogo kiasi hicho. Watoto wenyewe wengi walikuwa wanalia tu mda wote wanaita mama, sasa mimi kwa upande wangu nahisi haya ni kama mateso kwa mtoto, lakini mama anasema ni bora aende sasa ili ajifunze kukaa na watoto wenzake. Nyumbani tunapokaa watoto si wengi. Enzi zetu wengi tulikuwa tunaingia tukiwa na miaka mitano, ingawa wapo walioingia chini ya hapo kwa sababu maalum hasa kama shule ipo karibu sana na nyumbani. Shule tunayoweza kumpeleka ipo mbali kidogo na nyumbani kwahiyo kuna magari ambayo yatakuwa yanapitia watoto asubuhi saa moja na kuwarudisha saa tisa mchana. ndugu zanguni mliopitia kwenye haya hebu tupeni ushauri.