Umri halisi wa kumiliki gari kwa mwanaume na mwanamke!!!!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Posts
7,113
Reaction score
950
Niaje!!!!!!
Ndugu yenu mie nataka kujua kama kuna umri halisi wa kuanza kumiliki gari la kutembelea(sio pickup wala gari ya biashara)kwa mwanaume na mwanamke,kama zipo jee sababu za msingi za kumiliki gari?

Na jee umri huo ukipita jee habari ya gari ni kupotezea?



Nawasilisha.
 
Duh hapo tunaingia kwenye mipango ya mtu mwenyewe.
Mie mpango wangu upo nipate gari karibuni sitaki niukwae ubaba ndo niwe na gari.
Alafu gari ni anasa.
 
Yes!
But nijuavyo mimi kuna makundi matatu juu ya hili.
1.Under 30yrs old kwa mwanaume na under 25yrs old kwa mwanamke.

2.Under 40yrs old kwa mwanaume na under 35yrs kwa mwanamke.

3.Under 50yrs kwa mwanaume na under 40yrs kwa mwanamke.

Nikianza na hilo kundi no1,hili ni hot age,hapa kinachotumika ni fashion life.
Kila mtu huwa anataka kuonekana anazo na hata mavazi yake huwa smart,na ata gari lake pia huwa smart na pia anaweza lifungia mziki mkuuubwa na tv,na mara nyingi hutumia magari ambayo ni new model saloon cars.

Kundi no2:hapa huwa ni ile kumalizia ujana,mara nyingi huwa mtu analazimisha japo apate gari la bei ya chini ili nae aingie kwenye record ya kwamba aliwahi kumiliki gari,mara nyingi hupenda kutumia magari aina ya family cars maana huwa tayari kishaingia kwenye majukumu mengi ya familia.

Kundi no3:Kundi hili ndilo huwa hitimisho la umri wa kuisaka shillings.
Mtu huwa makini sana hapa ili asiweze kuanguka,na kama ni gari ya kutembelea basi sana sana ni gari ambazo ni economic car zaidi,mara nyingi hutumia escudo na single pickup!

Hayo ndio nijuayo mimi ingawa pia bado sijamiliki gari na umri wangu ni katikati ya 30-40!!!!!
 
nimemiliki gari la kwanza toyota mark 2 nikiwa na miaka 21,lilikuwa bovu hasa likipanda mlima hata mtoto anayetambaa anaweza lizidi.
 
Inategemea na mazingira na nchi,wenzetu gari sio utajiri wala ufahari ni kitendea kazi au miguu,
Sidhani kama kuna umri kamili wakumuliki gari,
Nakumbuka nikiwa na umri wa 24 tu nlikuwa namiliki Scania 113 mpaka jamaa nliokuwa nafanya nao business wananiita tajiri mtoto,japo sikulipenda jina hilo kwa sababu umri huo nlikuwa tayari nina mke na mtoto kwa hiyo sikuwa mtoto, gari haina umri ndugu yangu,nachoamini uwe kwenye age ya kisheria kupata leseni tu
 
Sidhani kama kuna umri maalum, ni maamuzi na uwezo tu wa mtu.
 
hakuna formula kwenye hili, kama kipato kinaruhusu hata ukiwa na 15yrs unaweza kununua mchuma, tatizo litakuja kwenye umiliki maana vielelezo/nyaraka zinasema umri juu ya miaka 18 maana wanaamini tayari ni mtu mzima na utaweza kuelewa vigezo na masharti. huwezi kupewa TIN number na TRA kama huna miaka 18 na kuendelea, hata leseni ya udereva. kama akili imekomaa na umri wako unaruhusu unaweza kuwa mmiliki halali, hii ni tofauti na mali za urithi
 
umri wowote ni poa, inategemea na mazingira!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…