SoC01 Umri sio Kigezo Cha kutuzuia tusifanye mabadiliko katika nchi yetu

SoC01 Umri sio Kigezo Cha kutuzuia tusifanye mabadiliko katika nchi yetu

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 29, 2021
Posts
81
Reaction score
158
Siku zote kinachotufanya tushindwe maishani, ni ile tabia kujiona mdogo na hivyo huwezi kufanya chochote.

Pale unapojichukulia kuwa wewe ni mdogo, huna sifa, ni dhaifu, na huwezi kufanya Jambo fulani, unakuwa unakosea. Na hii ndio sababu vijana wengi wa kitanzania huwa hatufanyi chochote au kusema chochote pale ambapo kitu kinapotokea au wanapoona kitu hakiendi sawa. Ile hofu ambayo vijana wa kitanzania tunayo yakuwa sisi ni vijana tutafanyaje ndio kwanza tupo chuo.

Mimi Ni kijana wa field ambaye nafanya kwenye kampuni fulani, nilivyokuwa ninaongea na mteja iliniweze kumuunganisha na huduma ya simu banking, alikataa lakini haikuishia hapo nilitaka kujua sababu ya yeye kukataa ndipo akawa ananieleze kuhusu makato na makato mapya yaliyotangawa kwaajili ya huduma za kibenki. Tulivyokuwa katika maongezi alisema kuwa inabidi sisi watu wa benki tuweze kutoa maoni na kuishauri serikali ili iweze kupunguza hizi Kodi.

Nilisikiliza kwa makini na ukifikiria kweli kama kuna watu ambao wakitoa mawazo kwa serikali na yakasikiliza au yakawa na ka uzito kidogo ni benki. Embu jiulize kama benki zote zilizopo hapa Tanzania kuanzia, AKIBA,NBC, CRDB, NMB, STANDARD CHARTER, na nyinginezo, fikiria kama hizi benki zikija pamoja na kutoa maoni na kuishauri serikali unadhani hazita sikilizwa? Kwa upande wangu , nadhani watakuwa na nafasi kubwa, kwasababu zile ni taasisi ambazo serkali inazitegemea sio kwa Kodi tu, na kwaajili ya ajira pia.

Sisemi kuwa wakifanya hivyo tozo zitapunguzwa wakati huo huo la hasha. Lakini Ni bora kutoa maoni kuliko kukaa kimya.
Kwakuliona hili nikaamua kushirikisha rafiki zangu wa karibu. Kiukweli walinicheka Sana. Mmoja alisema , “ kitu ambacho bunge limeshindwa kufanya wanachuo watano ndo tuweze!” Niliumia sana kwa hayo majibu lakini niliumia sana kwasababu ya jinsi walivyojichukulia.

Kama mwanafunzi wa chuo anajiona ni mdogo sana na hawezi kufanya chochote cha kutatua tatizo au changamoto inayoikabili jamii yake.
Usidhani kwamba mimi sijui kuwa hili ni jambo la kuishawishi serikali ni kazi ngumu sana kama sio kazi isiyowezekana kabisa, najua. Na hata nilivyokuwa ninawaambia wenzangu nilikuwa sijiamini hivi kwa kuwa nilikuwa naona tatizo hili haliko katika uwezo wangu lakini hata hivyo haimaanishi kuwa siwezi kutoa mawazo yangu ya jinsi ninavyoona hili tatizo linaweza kutatuliwa.

Kama msemo wa kizungu unavyosema , “Impossibility of a task should not discourage you from doing it” kwamba ugumu wa jambo kusikuzuie wewe kulitenda hilo Jambo. Atakama wenzangu walinicheka na kunidhihaki, mimi nilienda kwa Meneja wa benki ninayoifanyia field nikaongea nae, na chakushangaza alinisikiliza vizuri tu. Nilimuuliza kama hili Jambo linaweza kufanyika, aliniambia inawezekana lakini ni mlolongo mrefu sana.

Sisi kama ni taifa la kesho tutainuaje nchi yetu kama hatuwezi hata kuchukua hatua ndogo ambayo inaweza kuleta mabadiliko chanya katika nchi yetu? Hii ndio inasababisha hata tunapopata nafasi ya uongozi, badala ya kuiinua nchi tunaishusha kwakuwa tunyaona matatizo badala ya kuyatatua au hata kutoa mawazo, tunakaa kimya na kujijali wenyewe na matumbo yetu.

Lakini mimi nawasihi vijana wenzangu kuwa, tuna wajibu, na sio ombi ni wajibu wetu kuweza hata kujaribu kutatua changamoto ambazo jamii yetu na nchi yetu kwa ujumla. Na pale unapojiona mdogo kufanya jambo, kutoa wazo ili kutatua tatizo kumbuka kuwa, Mtumishi wa Mungu Daudi alimpiga Goliati akiwa ni kijana mdogo sana, na mtumishi wa Mungu Musa aliitwa kufanya kazi ya Mungu akiwa ni kijana mdogo pia, Samweli mtumishi wa Mungu naye aliitwa kwenye bibilia akiwa mtoto kabisa na mtumishi wa Mungu Yeremia vilevile aliitwa na Mungu akiwa na umri mdogo sana.

Kwahiyo umri sio Kigezo Cha kutuzuia tusifanye mabadiliko katika nchi yetu.
 
Upvote 5
Back
Top Bottom