Umri unaenda sijisikii kabisa kuoa

Umri unaenda sijisikii kabisa kuoa

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Umri wangu ni miaka 34 kwa sasa, Nina kazi as mwalimu, nafanya biashara na kilimo sana, nina nyumba zangu nilizojenga na nyingine za urithi, Nina mtoto mmoja namhudumia, mzazi mwenzangu nilishamtolea mahali yote kifupi kwa maisha ya kitanzania kwangu si Haba sana.

Changamoto niliyonayo kubwa kwa sasa sijisikiii kabisa kuishi na mwanamke najikuta muda mwingi nawaza fedha na Mali(kifupi nipo busy sana na kazi zangu ), huko nyuma nilikuwa kicheche sana na hadi nafika umri huu sijawahi kuishi na mwanamke kwangu zaidi ya siku mmoja(afike apigwe aondoke), mzazi mwenzangu aliponisumbua sana kuwa anataka tuishi as mke na mume nilimpeleka kuishi mmoja ya nyumba zangu.

Huwa nakwenda hapo Mara moja moja wikiend na Siku moja moja za kazi nikiwa free napumzika nakwenda hapo,kifupi sina call kabisa ya kuishi na mwanamke seven days of a week, mbaya zaidi mzazi mwenzangu kanipa masharti hatobeba mimba hadi tuishi wote, na Mimi natamani watoto wingine sana Ila kuishi na mwanamke sioni wito kabisa nifanyeje, najikuta nawaza kuzaa na mwanamke mwingine nimpe fedha anizalie tu lakini habari ya kupiga kambi pamoja haikaai akilini mwangu, wadogo zangu wanaoa , marafiki zangu wanaoa ila Mimi naona wito sina kabisa.

Nifanyeje maana naanza kuiogopa hatma yangu
 
Listen to your heart. Kutokuoa sio dhambi, kwamba utahukumiwa. Cha msingi,ujiridhishe tu kuwa ndoa sio wito wako, usijefika 45+, dakika za nyongeza, ndo uanze kuwaza kuoa na kuzaa, utakuwa umechelewa (kwa mtizamo wangu). Kumbuka, kulea familia hakuhitaji pesa pekee, nguvu za mwili na uwepo wako vinahitajika sana
 
Kusema kweli huu uzi naona umejielezea na umejijibu kwanini mleta uzi yupo hivyo.

Hapa labda tuanze kuleteana masikhara.
 
Zaa na huyo huyo mwanamke kuliko kutoka nje kuzaa na mwanamke mwingine... Hapo utakuwa unaongeza balaa juu ya balaa
 
Back
Top Bottom