Asa sjui mambo ya nguvu za kiume ila nadhani watu wengi wanakwepa ile hassle ya kuhangaika na mtoto mkubwa anapokuwa na likidonda,pengine hata kujitonesha.
pia usumbufu wake kwanza mpaka mfikie muafaka wa yeye kukubali kutahiriwa vita yake kwahiyo mwishowe mnaishia kumchoma masindano ya usingizi wakati kumtahiri na madaktari wanadai si nzuri.
Siku izi mtoto anatahiriwa hata ndani ya wiki baada ya kuzaliwa,ila angalizo:daktari awe na uzoefu wa kufanyia watt wachanga la sivo itakua shida,wakifanyiwa kipindi hicho anapona ndani ya siku 7 na diapers anavaa kama kawaida akishatairiwa kuna dawa flani kama cream unakuwa unampaka ili kidonda kisinatie kwenye diaper na panadol anakunywa basi.
ila sio guaranteed kuwa kila mtt mchanga atakubaliwa kutahiriwa,hayo ni maamuzi ya daktari akishamwangalia ndo anaamua kama atatahiriwa au la.