Jamani umri wangu naona kama unasogea taratibu,nina miaka 42 lakini sijaoa bado,lakini niliishi na mwanamke miaka ya nyuma tukazaa lakini tulipoachana mpaka leo sijafikiria kuoa tena,lakini nahisi nimejiandaa kupambana na uzee peke yangu,kuna ushauri?
Ndugu
Hata ulivyojieleza ni matatizo matupu
Huyo uliyeishi na kuzaa nae ulimuoa?? Mliachana kwa sababu zipi, na wakati gani?? Au ulimpa mimba akiwa shule???
Sasa uzee utaishiji peke yako?? Ukiumwa nani wa kukupeleka hospital?? Ukistaafu nani wa kukutunza?? Au unafikiri pensheni haiishi???
Badilika bana, wanawake wamejaa kibao siku hizi.
Ila tahadhari! Sio vyote vin'gaavyo ni dhahabu.
Jaribu kumfahamu kwanza mwanamke kabla ya hatua yoyote.
mambo yako ya ajabu kama Avatar yako!!!
nitafute wa umri upi?hakuna kitu nachukia kama kupigiwa mkeo,nisije zeeka yeye bado anadai
Jamani umri wangu naona kama unasogea taratibu,nina miaka 42 lakini sijaoa bado,lakini niliishi na mwanamke miaka ya nyuma tukazaa lakini tulipoachana mpaka leo sijafikiria kuoa tena,lakini nahisi nimejiandaa kupambana na uzee peke yangu,kuna ushauri?
Tulia bado umri unaruhusu tafuta mwenye kukufaa ila kumbuka sio kila mwanamke ni mke, usije kurupuka ukaangukia koroma. Mwombe mungu akufungue na umpate mke mwema.
Ila kumbuka watoto ulionao ni wakwako na mke wako pia usiwasahau
CPU,umetoa ushauri wa hekima sana,isipokuwa tu kwenye hizo red,hayo mambo siku zote ndo huwa nayakataa,'kuoa kwa sababu ya....',hapa unaongelea kuoa kwa sababu ya kukwepa upweke uzeeni,kuwa na nesi wa uhakika,kutunzwa....jamani hizi ndizo SABABU za kuoa kweli? ina maana kama nina invest kwenye 'nursing home' nikalipia pesa kabisa wakati wa ujana wangu basi kwa msingi huu sitakuwa na sababu ya kuoa kwa sababu uzee wangu uko secured?Ndugu
Hata ulivyojieleza ni matatizo matupu
Huyo uliyeishi na kuzaa nae ulimuoa?? Mliachana kwa sababu zipi, na wakati gani?? Au ulimpa mimba akiwa shule???
Sasa uzee utaishiji peke yako?? Ukiumwa nani wa kukupeleka hospital?? Ukistaafu nani wa kukutunza?? Au unafikiri pensheni haiishi???
Badilika bana, wanawake wamejaa kibao siku hizi.
Ila tahadhari! Sio vyote vin'gaavyo ni dhahabu.
Jaribu kumfahamu kwanza mwanamke kabla ya hatua yoyote.
ana matatizo kivipi?Daah! mi nahisi unamatatizo mzee, hebu kawaone wataalamu kwani unaweza ukawa unajiona upo sawa kumbe unamatatizo
bishanga naomba wanilewe,sina tatizo lolote ila nahisi naona labda sio lazima kuoa thats all