Mkuu, wapo hata kama ni wachache ambao husubiri mpaka wafunge ndoa ndiyo wafanye tendo la ndoa. Sisi inafaa kuwafundisha watoto wetu kilichoadilifu hata kama sisi wenyewe tulishindwa. Si unafiki. Kushindwa kwetu kusitufanye tuache kutimiza wajibu wetu. Watoto/vijana wana haki ya kuujua ukweli wanaopaswa kuuishi. Na hata pale wanapokwenda kinyume wajue wamekosea/ wawe answerable.
Watoto/vijana tunawafundisha wasubiri kwa sababu:
1. Kimaadili si sahihi kufanya ngono nje ya ndoa.
2. Wanakuwa pia na majukumu yao, mf. masomo ambayo yanahitaji utulivu wa akili na concentration. Ngono wakati huo inaweza kumharibia masomo mf. kupata mimba kwa mtoto wa kike, au kwa mvulana kupata mtoto kwa mpenziwe kabla ya kuwa na uwezo wa kumlea, nk. They have to be one at a time. Mabo mengine yatakuja kwa wakati wake.