Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Mimi huwa nashangaa watumishi kuchukulia maneno ya Musa (Zaburi ya 90:10) na kuacha neno la Mungu mwenyewe la (Mwanzo 6:3) "Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini." (Yaani miaka 120)
Sasa watu wengi wakiongozwa na watumishi wa Mungu wamekomaa na Zaburi 90:10.
Ukitaka kujua maana ya huu mstari wa Zaburi 90:10, anzia kusoma mstari wa 5 hadi 12. Hapa anaongelea maisha ya mtu anayeishi katika dhambi, mateso na maangaiko huku hasira ya Mungu ikimkalia huwe na uhakika huwezi fikisha miaka 120. Lakini ukiishi kwa kufuata kanuni za kihistaarabu na kiungwana ukaachana na umalaya, pombe za kupindukia, vyakula visivyofaa, ukafanya mazoezi, ukaheshimu wazazi wako, ukatii mamlaka za nchi, ukatumia akili sawasawa ulizopewa na Mungu (maana wengi hatutumii hata 1% ya akili), ukamcha Bwana, ukajitenga na migogoro ya kuhamsha hasira za waliokuzunguka wasikuroge au kukudhuru, ni lazima utaishi hiyo miaka! Wachungaji semeni ukweli wa huu mstari wa Mwanzo 6;3. Miaka Mungu aliyotuhahidi ni 120 au angalau ukaribie! Wengi wanazima moto ndani ya miaka 70-80 kutokana na kuaminishwa na laana ya mdomo maana maneno yanaumba! Kataa hii laana! Sema mimi nitaishi miaka 120 aliyosema Mungu katika jina la Yesu!