Umri wa kuishi aliosema Mungu mwenyewe kwa kinywa chake ni miaka 120. Kwanini mnakomaa na miaka ya tabu ya 70-80?

Imani sio dini. Ni kama vile ambavyo unashindwa kuelewa uumbaji wa dunia. Ni kama vile ambavyo huelewi mtu akifa anaenda wapi.
Kuwa na akili ni pamoja na kuamini mambo makubwa ambayo mpaka sasa hayana majibu. Tulia mwabudu Mungu.
 
Vyakula tunavyo kula.life style tulip ivumbua na majanga ya kibinadamu..wachache tena walio zawadiwa umri mrefu ufika mpaka 120,lakini wengi wetu 60-70..
 
Nadhani hakupata memo na kuwapiga waliotumikisha bara la Africa au wakati hata Yesu utumwa unaendelea nadhani ulikuwa ni Kosher...
Nadhani haujaelewa point yangu ungeelewa tangia mwanzo ni kwamba alijua kwamba watamkosea na watalalamika kwahio that should never have been a surprise na unaposema alikasirika unaanisha alikuwa emotional kwa kitu ambacho aligundua from the get go ?
Again this is neither here nor there tunazidi kuongeza maswali badala ya majibu and you are painting the picture kwamba Mungu ni emotional na anatak reciprocation, na kufanya vitu kwa shuruti (sasa tukubaliane kwamba kama anafanya vitu kulinganisha na happenstances basi kesho haijapangwa sababu kama waisrael kama unavyosema wasingemdharau asingekasirika na asingepunguza miaka yao)
Kwahio hapo ni kama aliwapa adhabu au zawadi ? Sababu kama tunaamini Mbinguni ndio all that si tungepunguziwa kabisa hata tuishi miaka kumi ili tuwahi safari ?
Kwahio kwa ufupi hakuna miaka iliyopangwa hio 70/80 kama yardstick duniani sababu huenda tunasoma kitabu cha waisrael tunakileta kwa wahindi wenye Imani zao, Na hii inaleta loophole sababu how do we know hapa anaongea na waisrael na wapi wengine wanajumuishwa
Kufa kwa uzembe ni kufa kwa uzembe sio kila kifo ni mpango wa Mungu haijalishi anakufa akiwa mtoto au mtu mzima
Ungesema haya tangia mwanzo wala tusingebishana mimi ndio nasema tangia awali kifo kipo mikononi mwako au uzembe wa waliokuzunguka unless umezeeka na organs zimechoka (what lives must die)
Sasa kama hapa tumeingia kwenye Imani wala siwezi kukubishia hata ukiamua kuamini kwamba dunia hakuna kinachoendelea na ni ndoto hakuna mtu yoyote ni wewe pekee na hii dunia is your imagination, sitaweza kubisha (sababu ndicho unachoamini wewe binafsi)

Na unless unaamini kwamba Mungu hajui kesho na kinachotokea kwa wakati husika ndio ana act basi your premise has a lot of fallacies...
 
CHADEMA hao, siyo sisi
 
Hakuna Mungu aliyesema watu waishi miaka 120.

Hakuna Mungu anayepanga umri wa maisha ya mtu.

Watu wengi wanakufa kutokana na ujinga, uzembe, kuishi kwa mazoea, ukosefu wa maarifa na umaskini.
 
Hakuna Mungu aliyesema watu waishi miaka 120.

Hakuna Mungu anayepanga umri wa maisha ya mtu.

Watu wengi wanakufa kutokana na ujinga, uzembe, kuishi kwa mazoea, ukosefu wa maarifa na umaskini.
Kwahiyo watu wasio wajinga ambao sio wazembe na wasioishi kwa mazoea na wenye maarifa wanaishi hadi miaka mingapi?
 
Imani sio dini. Ni kama vile ambavyo unashindwa kuelewa uumbaji wa dunia. Ni kama vile ambavyo huelewi mtu akifa anaenda wapi.
Nani amekwambia hayo hayaeleweki ? Wewe kama huelewi ni wewe, Ila kama unaamini chochote kile pia ni Haki yako binafsi na wala siwezi kujaribu kukupinga unachoamini, I can only debate / speak on facts hayo mengine siwezi nikakubishia...

Na uzuri wa facts tunaelewa kabisa kwamba kuna known knowns na known unkowns (hatuhitaji kutunga uwongo au kujiridhisha kwa chochote ambacho hatukielewi kwa ku fill in the blanks) kufanya hivyo ni kujipa majibu rahisi kwenye mambo magumu
Kuwa na akili ni pamoja na kuamini mambo makubwa ambayo mpaka sasa hayana majibu. Tulia mwabudu Mungu.
Moja hakuna mtu ambae hana akili na kila mtu anaweza kuamini anachoamini na kutokuwa na majibu sio kuchukua jibu unaloambiwa na fulani au watu wa mahali fulani bali ni kuendelea kuchunguza ili zile known unkwons kuzibadilisha kuwa known knowns....

As kumwambia mtu mwabudu Mungu ndio hizo naita indoctrination binafsi siwezi kumchagulia mtu cha kufanya nachoweza kumpongeza ni kuendelea kufanya utafiti wa kufahamu known unknowns..., na sio kumpa jibu ili aende kutafuta swali....
 
We mwenyewe unaona kwamba you are addicted to certain things which are killing you.
Halafu una complain kuhusu life expectancy ya humans.
 
Nadhani hakupata memo na kuwapiga waliotumikisha bara la Africa au wakati hata Yesu utumwa unaendelea nadhani ulikuwa ni Kosher...
Mungu hakuwatoa Israeli utumwani kwa sababu TU aliwaonea huruma, ziko sababu kadhaa za kwa nini alichagua kushughulika na Israeli ijapokuwa kulikuwa na jamii nyingine za kitumwa. Kusema unadhani hakupata memo inadhihirisha umeamua kudhihaki, and that raises a red flag as to whether or not you are willing to learn anything.

Nadhani haujaelewa point yangu ungeelewa tangia mwanzo ni kwamba alijua kwamba watamkosea na watalalamika kwahio that should never have been a surprise na unaposema alikasirika unaanisha alikuwa emotional kwa kitu ambacho aligundua from the get go ?
Ok, upande mmoja wa swali lako sio mwepesi kujibu maana hakuna mwenye majibu ya moja kwa moja, tunachojua ni kwamba pamoja na kwamba Mungu anajua yote lakini amemwumba mwanadamu kuwa na utashi wake binafsi, kwa hiyo Mungu huwa ana tabia ya kumshirikisha mwanadamu katika kutekeleza mapenzi yake lakini mpango wake utakamilika kwa namna nzuri (kama mwanadamu alitii sauti ya Mungu) au kwa hata namna mbaya(kama mwanadamu hakutii sauti ya Mungu).

Mungu alimwumba mwanadamu na uwezo mkubwa wa kimaamuzi lakini Mungu hubaki kwenye nafasi ya kuruhusu au kutoruhusu jambo la mtu. We are not programmed species but that does not make our creator less of a God.

Nilikupa mfano kama wewe ni baba na unahudumia mtoto wako vizuri kimalezi, kimatunzo, kiulinzi n.k. Halafu mtoto anakua huku akikudharau akisema wewe si baba yangu na akikuonesha tabia mbovu, wewe hutamwadhibu? hutakasirika? Kama wewe utakasirika na kumwadhibu mwanao kwa nini iwe tatizo kwa Mungu, na Biblia inasema tuliumbwa kwa mfano wake?

Kwahio hapo ni kama aliwapa adhabu au zawadi ? Sababu kama tunaamini Mbinguni ndio all that si tungepunguziwa kabisa hata tuishi miaka kumi ili tuwahi safari ?
Ni adhabu, na kudhihirisha ni adhabu baada ya tangazo la hiyo adhabu waliomboleza sana, kitu chochote chaweza kutumika kama adhabu ikiwa kitaumiza hisia zako. Mwanadamu hakuumbwa ili akaishi mbinguni, mbinguni ni makao ya Mungu na hata baada ya ukamilifu wa nyakati kutakuwa na mbingu mpya na nchi mpya kwa ajili ya mwanadamu.

Ndio, kuna uwezekano mkubwa tu wa kuhubiri kitu ambacho si sahihi, japo hili si jambo la msingi sana kiimani kwa hiyo hata mtu akikosea katika kufundisha na dhamiri yake ikiwa safi haiwezi kuwa dhambi, Hatuna uelewa sawia kwa kila mstari wa Biblia japokuwa Imani yetu juu ya mambo ya msingi inaweza kuwa unafanana.

Ungesema haya tangia mwanzo wala tusingebishana mimi ndio nasema tangia awali kifo kipo mikononi mwako au uzembe wa waliokuzunguka unless umezeeka na organs zimechoka (what lives must die)
Bado Mungu ni mwenye final say juu ya kifo cha mtu, unaweza kufa kwa uzembe wako, kwa uonevu wa shetani, kwa kutokujua/ujinga juu ya mambo fulani, au kwa siku zako kutimia. Kuna permissible will of God and perfect will of God, vifo vingi na hata matukio mengi yanatokea chini ya "Permissible will of God" kuliko perfect will of God.
 
Uzuri hawajakukataza kuishi miaka 120
 
Ayubu 14:1
[1]Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke
Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
Yohana 5:24
[24]Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.

Yohana 3:7
[7]Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
Ukizaliwa mara ya pili unazaliwa na mwanaume maana mwanadamu wa kwanza Adamu ndiye aliyemtoa Hawa,hivyo Hawa alizaliwa na mwanamke Ukizaliwa na mwanamke lazima siku zako za kuishi ziwe chache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…