Miezi 6 hujamkalisha mtoto, tena mtoto wa kike, umemchelewesha sana bibie, usije ukatuharibia mtoto bure, miezi 6 alitakiwa awe ameshakaza kukaa na akifika miezi 9 anaanza kutembea, hebu anza kumkalisha mtoto bana
Mtoto wa kike anawahishwa kukaa kuliko wa kiume.....wakike unaweza kumuanzisha hata akiwa na miezi mitatu taratibu,mpk akifika miezi sita anakuwa ameshakaza ...lkn wa kiume unaanza akiwa na miezi sita kumkalisha.
watoto wenye afya hasa wa kiume wanapenda sana kukaa mapema(hawapendi kubebwa kitoto toto) lakini usiwafuatishe wanavyotaka
mzurimie thanks mumy mimi sijamwanzisha bado hebu ngoja niache kyumwonea huruma nimkalishe kuanzia leo asije kua mzembe
Sorry, I meant 6+3=9. The logic is contained in the explanation. Asante kwa kukosoa.
uwiiii Mtende miezi sita wanaanza kutambaa hata kwenye kadi la klinic kwenye ile chart wanaonyesha kwa mtoto wa kike miezi mitatu unaanza kumbeba kwa kumkalisha 4 anakaza kabisa wa kwangu meno aliota na miezi mitano.
the secretay daah yani mnavyoniambia hivyo mnanipa moto maana since jana nimekua nikimkalisha tuu mpaka anachoka anadondoka mwenyewe ila ntahakikisha namkazania kwa nguvu zote japo nimeanza jana ila hawezi kukaa pekeak mpaka nimshikilie au nimwekee mito ajizuilie nayo
Tatizo siku hizi manalea watoto kidigital sana, anyway mkalishe kwenye kochi/sofa muwekee vimto pembeni ukimkazania within 1 to 2 wks ataanza kukaa mwenywe halafu sio akianza kulia tu unamnyanyua, utakesha nae, mwache akae hata akilia sometimes muache tu, kila kizuri kina gharama ati