Umri wa mtoto kuanza kutembea

Umri wa mtoto kuanza kutembea

nikupe hongera kwa kupata mtoto wa kwanza, lakini niseme pole kwa changamoto hiyo.
Namshukuru mungu, mwanangu amekuja tembea akiwa na miaka miwili na miezi 5.
Kwa sasa yuko vizuri kabisa.

ahsante kwa hongera, pole sana kwa mwanao kuchelewa kutembea. Mungu ni mkubwa
 
Hapana mtoto wa kike anaanza kukaa mapema kuliko mtoto wa kiume,mtoto wa kike ni rahisi kutembea mapema kuliko mtoto wa kiume,mtoto wa kike ni imara zaidi upande wa afya kuliko mtoto wa kiume.Mtoto wa kiume ni dhaifu zaidi kuliko mtoto wa kike.Mtoto wa kiume umri kati ya 0 - 1 year anahitaji uangalizi mkubwa zaidi ukilinganisha na mtoto wa kike.
mbona mtoto wa taifa tiffa hajatembea?
 
Kuna uwezekano pia tabia zenu wewe na mkeo. Kama mkifanya tendo la.ndoa mkalala bila kuoga nalo ni tatizo sugu kwa watu wengi. Au labla umekwisha mpa mimba nyingine mama yake nalo ni tatizo. Vyema awe na kitanda chake la sivyo atakuwa fundi viatu
kumbe ndo maana mtoto wa diamond hajatembea
 
kwamtoro heshimu hisia za watu wengine. Hiyo sentensi yako ya mwisho sio nzuri hata kidogo!!!
Sasa unataka wazazi wenzangu wasiambiwe ukweli? Unakuta mama ananyonyesha ila anawanaume huko nje/au kutwa usiku kusogezana na baba mtoto na akitoka Ku ndi ndi ndi huko anamnyonyesha mtoto hata Ku oga hajaoga, Kulea mimba si kazi-kazi kulea mwana wazazi tuwe makini imani dawa hata kama wataalam watapingana na hili
 
Huna haja ya kua na wasiwasi manake kama ameweza kukaa na kutambaa kuna wakati utafika na atatembea cha msingi ongeza lishe na kua karibu zaidi naye.
 
Swali lako la kwanza, hamna tofauti yeyote kati ya mtoto wa kike na wa kiume. Kikubwa ni matunzo na lishe bora kwa mtoto.Swali la pili, sijakuelewa

Kuna tofauti kati ya mtoto wa kike na wakiume, mtoto wa kike anawahi kuanza kukaa, kutambaa then kutembea, wakiume wanachelewa kiasi
 
kukaa aliwahi, kutambaa ilikuwa issue, kutembelea vitu ndiyo kaanza sasa. Ana mwaka na miezi saba

Angefikisha mwaka tu ungemtengenezea kigari cha mbao cha kusukuma, angeshatembea siku nyingi
 
Huyo mtoto tafuta pia kampani ya watoto wenzake ili wamchangamshe
 
Mtoto wa Diamond Yule mtoto wa Taifa ...sijui Tiffah ... Atakuwa ni mwanaume maana hajatembea mpaka leo
 
Nna mtoto wa kiume ana miezi 7 na kaanza kukaa na miezi 4-5.... Nimemnunulia babywalker na kwa sasa anazunguka tu ndani vurugu tu mara huku mara kule .... Kutembea ni malezi tu.... Mnataka kutuletea za kizamani oooh mjamzito haruhusiwi kula mayai ya kuku.... Pyeeeeeee😛
 
Nna mtoto wa kiume ana miezi 7 na kaanza kukaa na miezi 4-5.... Nimemnunulia babywalker na kwa sasa anazunguka tu ndani vurugu tu mara huku mara kule .... Kutembea ni malezi tu.... Mnataka kutuletea za kizamani oooh mjamzito haruhusiwi kula mayai ya kuku.... Pyeeeeeee😛
baby walker inaharibu watoto miguu atakuwa na tege mpaka utashangaa wacha hyo kitu mkuu
 
Yap mtoto kutembea ni malez ucpende kukaa muda wote yu mikonon pia mpe muda wa kucheza na watoto wenzie ili aone wiv
 
Kuna uhusiano gan kati ya haya ..... Kipindi cha mama anapokuwa n mjamzito akatoka nje ya ndoa au mme kutoka nje ya ndoa pindi mwanamke atakapofikia kipind cha kujifungua uchungu humsumbua na hupelekea hata mtoto kufa acpopewa mama huyo dawa au akinusurka huambulia kupasuliwa tuuuuuu
 
Kivp mkuu, tuelimishe.. Maana hata wangu anatumia sana hcho
th
th
 
Back
Top Bottom