Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Jana nilikutana na mzee wa miaka 92 akiwa mzima bukheri wa afya. Alikuwa ameongozana na binti yake wa miaka 65. Mwanzoni nilifikiri ni mke wake, ni baada ya kusikia maongezi yao mama yule akitamka “baba”. Nilifikiria hivi ni wangapi wa umri huu wana fahari ya kuita neno baba, mama.
Nilipata wasaa wa kuongea nao. Mzee alistaafu enzi za awamu ya pili. Mke wake alifariki miaka 10 uliyopita, walijaliwa kupata watoto watano na wote wako hai.
Mzee akili yake imetulia kabisa na aliweza kuniambia kwa furaha baada ya kustaafu walipata nafasi ya kushiriki mikutano ya Injili sehemu mbali mbali na mke wake. Wamekwenda Kenya, Uganda, Afrika ya Kusini .
Nilivyo mbea nilikuwa mdadisi, mzee alilima mboga zake nyingi mwenyewe lakini uwezo huo sasa umepungua. Anaishi mwenyewe na mtu wa kumsaidia na watoto wanamtembelea kila mara kwani karibia wote wamesha staafu.
Ni baraka kufika 90* ukiwa na nguvu na akili timamu.