Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habari za wakati huu;
Maisha ni safari. Katika safari hii tunapitia mengi,mema na mabaya.Wakati mwingine kuna ambayo yanatupata ambayo tunaweza kuyazuia/kuyafanya yawe vile tupendavyo na kuna wakati yanakuwa nje ya uwezo wetu. Ili kuishi maisha yako ni muhimu na lazima kuwa na mipango au malengo. Wengi sana hukwama au hufanya uzembe katika eneo hili la mipango na kujikuta wakiishi maisha ya kuiga,kukurupuka, kulaumu, kujilaumu na kujuta.
Naamni kabisa kwamba mpaka kufikia umri wako unaelewa nafasi au mahali ulipotoka,ulipo na unapoelekea.Hivyo basi ninapozungumzia kuweka mipango ya kimaisha unaelewa ninachomaanisha.
Mimi binafsi nimeanza kuwa na mipango ya maisha tangu nikiwa kijana mdgo sana.Kila mwaka nilikuwa nikiwa lengo la kuhakikisha kwamba ninaishi mpaka nione mwaka unaofuata.Nilikuwa naogopa sana kuweka malengo na hata pale nilipojaribu kuweka malengo sikuyatilia maanani kwa sababu sikuliona kama ni zoezi la muhimu katika maisha yangu.Kadiri nilivopata hekima na kimo nilijaribu kuweka malengo madogo na rahisi kutimia ili tu kujifunza kuweka malengo.
Ilikuwa ni rahisi kwangu kuweka malengo ya siku kuliko kuweka ya wiki,mwezi/mwaka.Najua wapo wengi ambao kwao zoezi la kuweka malengo ya mwaka ni zoezi lisilokuwa na maana na ni kama ndoto za alinacha ila leo natka nijaribu kuwaonesha faida na umuhimu wa kuweka malengo na namna bora ya kuyaweka malengo yako na kuyafikia.
Malengo yako katika maisha yanapaswa kuwa katika maeneo manne ambayo Malengo ya KIAFYA.KIUCHUMI,KIJAMII na BINAFSI
Malengo ya Kiafya yanahusiana na afya yako kwa aujumla kuanzia maradhi,lishe,mazoezi,afya ya akili etc.
Malengo ya kiuchumi yanahusiana na masuala ya uzalishaji thamani,usimamizi wa fedha.utajiri,uwekezaji,ajira na biashara
Malengo ya Kijamii yanahusiana mahusiano yako ya kifamilia,kimapenzi na mahusiano yako na jamii kwa ujumla.
Malengo yako binafsi yanahusu zaidi hali yako ya ndani na binafsi kama vile kujiamini,kujipenda,kujiheshimu,kujithamini,kujielewa,kujielimisha na kujijali
Ili uwe na maisha makamilifu ni muhimu uweke malengo katika kila eneo kwa kuzingatia hali na nafasi yako ya sasa na matarajio yako ya baadaye.Unapoweka malengo fahamu kabisa kwamba haya maeneo yote yanategemeana na kama eneo moja likiwa na matatizo linaweza kuathiri maeneo mengine kwa kiwango kikubwa na kwamba moja ya jukumu lako ni kuhakikisha kwamba unaweka malengo ambayo yanategemezana kwa kila eneo yaani Malengo yako Bianfsi yaweza kusaidia kufikia malengo yako ya kiafya,kijamii na kiuchumi bila kuathiri malengo yako mengine.
Kabla ya kuanza kuweka malengo yako ni lazima ujipe muda wa kufanya zoezi hili.Kama una uwezo unaweza kutenga muda mrefu kama wiki kwa ajili hio au unaweza kutenga muda maalum kila siku kwa ajili hio.Vyovyote vile ni muhimu kuzingatia kwamba hili ni zoezi muhimu sana.
Ni muhimu pia ukatenga eneo maalum kwa ajili ya zoezi husika ambapo hakutakuwa usumbufu wa aina yoyte ile utakaoweza kuathiri utekelezaji wa jambo hili.
Andika katika notebook/karatasi/diary yale malengo muhimu ili uyasome na kuyapitia kwa kina na umakini.
Kwa kila lengo utakaloweka hakikisha unafahamu kwa kina iwapo lengo hilo litahitaji support ya watu fulani mfano wazazi,mwenza au watoto ili uweze kuwafanya wawe sehemu ya malengo yako.Jitahidi sana malengo yako yawe ndani ya uwezo wako,yaani yasitegemee sana watu wengine ili yatimie.
Unapoweka malengo usisahuhau ulipotoka na ulipo kwani unaweza kuweka malengo makubwa kuliko uwezo wako na kujikuta unajichosha bila sababu.Hakikisa unatambua uwezo wako halisi kwa kuangalia namna ulivotenda kwa mwaka unaoisha na kujipima kwa ukweli na haki.Ukishaweka malengo yako hakikisha kwamba unatambua yape utayafanya kila siku ili kufikia hayo malengo yako makuu.Yaani kama lengo linahitaji uweke akiba basi weka akiba hio kila siku,kama linahitaji ujifunza kitu kipya basi jifunze hicho kitu kidogo.
Mimi naamini kabisa ktika kujifunza kidogo kidogo.Kwa mfano lengo langu ni kuja kuwa mwandishi wa vitabu,Ili kufikia lengo hili lazima nijifunze kuandika,Kwa sababu natambua kwamba JF ni sehemu tumepewa kuweka maandiko yote ni kupata wasomaji wa haraka basi huwa najitahidi kuandika makala tofauti mara kwa mara na kuangalia muitikio wa wasomaji na mimi mwenyewe kusoma makala zangu na kuona ubora wake.
Kwa kufanya hivi nimekuwa nikiboresha mtindo na uwezo wangu wa kuandika kidogo kidogo.Kadiri siku zianvoenda napunguza typo errors,etc na speed yangu ya kuandika andiko imeongezeka kiasi kwamba naweza sasa kuandika andiko kama hili kwa muda wa dakika 30,kuwaza,kuchapa na kulirusha kwako ulisome.
Haya mazoezi madogo hujenga matokeo makubwa kadiri muda unavoenda na unaweza fanya hivyo katika kuacha tabia mbovu.kujenga tabia mpya,kujifunza ujuzi mpya,kujenga desturi mpya na hata kubadili namna yako ya kufikiri.
Sisemi kwamba ni rahisi ila inawezekana kabisa.
Kwa kupitia maandiko yangu humu JF kwa mwaka huu wa 2020 nimekutana na marafiki wengi wapya,nimeongeza kipato chango maradufu,nimejifunza mambo mengi,Nimetembelea zaidi ya mikoa 16 ya Tanzania kwa sababu tu ya baadhi ya maandiko na matangazo mbalimbali na matumizi ya Ujuzi wangu.Nimejifunza kwamba inawezekana kutumia ujuzi na uzoefu wako kuongeza kipato na kuwasaidia wengine katika masuala mbalimbali huku ukiisha maisha ya amani na utulivu.
Kwa kupitia njia hii hii ya kujifunza taratibu,kuweka malengo na kuyafanyia kazi taratibu nimesaidika sana.Nimeweza kupewa Complementary Holidays katika kisiwa cha marashi cha Zanzibar kwa sababu ya watu ambao niliwafurahisha/kuwasaidia kwa namna moja au nyingine kwani kuna mambo ambayo mimi huyaona madogo au na marahisi lakini kuna watu yanawasumbua na kuwatesa na ukiweza kumsaidia anajisika furaha sana.
Katika kuweka malengo yako ya mwaka usishau kuweka lengo la kiafya linalohusisha kuwa makini na aina ya vyakula na ulaji kwani ulaji wetu unachangia sana matatizo yetu ya kiafya
Katika kuweka malengo yake ya binafsi usiache kuweka lengo la kujifunza kitu kipya katika fani au taaluma yako au taaluma nyingine kwa maarifa ni moja kati ya njia bora ya kuongeza furaha na kujiamini
Katika kuweka malengo yako ya kiuchumi usisahau kuweka lengo ama la kuanzisha biashara,kuweka akiba,kuwekeza au yote kwa pamoja.Hili ni moja kati ya eneo ambalo linakufanya uongeze uwezekano wa wewe kuwa na uhuru wa kiuchumi
Katika kuweka malengo yako ya kijamii hakikisha unaweka lengo la kunetwork na watu sahihi na kupunguza idadi ya marafiki ambao wanaongeza matumizi,kupunguza mapato na kukuongezea stree,Jitahidi uwe na marafiki wa chache huku ukiwa na mtandao mkubwa watu wanaoweza kukupa fursa na unao weza kuwapa fursa.Unaowapa fursa watakuja kukupa fursa wewe ili usikubali kuzungukwa na machawa.
Kama nilivyosema huu uzi ni mrefu na nimeuandika kwa muda mfupi kama sehemu ya mazoezi.Iwapo umependa nilichoandika na kimekusaidia unaweza pia kumshirikisha mtu mwingine kwa kutoa credit,iwapo kuna kitu unaona kitawafaa na wengine ongezea kwenye comment uwasaidie watu waishi maisha bora.
Kama Uzi umekuboa nisamehea kwani hata kusoma nako kunahitaji mazoezi kidgo kidogo na uanweza kuweka kama lengo lako la 2022 kwamba uweze kusoma nyuzi ndefundefu.Unaweza kujikuta unaweza kusoma hata kitabu kizima na kukimaliza.
Kama huna maoni wala ushauri basi tukumbukane katika maombi.
Nawatakieni wakati mzuri na wenye furaha