Umuhimu wa binadamu kujipenda

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ni muhimu binamu kujipenda, kuanzia usafi wa nywele, ngozi, kinywa, mavazi , malazi na chakula. Kwenye bible Adams alipewa nguvu na uwezo wa kutawala wanyama sasa tusipojipenda si tunajiweka sawa na wale tunaowatawala?

Nywele ni muhimu zisafishwe kwa uchache mara moja kwa wiki. Kinywa kisafishwe kwa uchache mara mbili kwa siku lakini kuna wanaobeba muswaki kwenye handbags na wanasafisha kinywa hata wakiwa kazini baada ya lunch.

Ngozi inatakiwa kuoshwa angalau mara moja kwa siku na kupakwa vilainishi, hivi hii fanya ngozi kuwa laini na ya kuvutika. Kumbuka kuwa kuna uchafu wa mwili unaotokea kwenye ngozi. Kwahiyo katika masaa 24 ni vyema kuitendea haki ngozi yako kwa maji na sabuni.

Usafi wa nguo za ndani zilizokuwa nguo zinapambana moja kwa moja na ngozi kama pichu, vest, sidiria, socks na boxer hivi vinatakiwa kubadilishwa kila siku.

Shuka za kitandani angalau Mara moja kwa wiki.

Deodorant inasaidia unadhifu hii ni inapaswa kutumika mara unapimaliza kuoga na kujikausha. Maisha ya boarding tulishare deodorant kutoka mwanzo wa bweni mpaka mwisho nikikumbuka ninacheka sasa hivi siwezi kushare deodorant na mtu labda spray lakini si roll on

Make up kwa sisi mabinti wa Hawa, ukirudi jioni unaoga na kupaka moisturiser tu kuipa ngozi nafasi ya kupumua. Unamkuta mdada ametoka kazini amefakamia mipombe akifika nyumbani analala hivyo hivyo. Eti nae anataka aitwe Lady.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Ahsante my dada kwa somo zuri lenye kufundisha. [emoji122] [emoji122]

Kama hiyo ya makeup walio wengi hawajui kama uso unatakiwa kupumua saa nyingine , na hata kama wanajua katika walio wengi wanaopaka ni wachache wenye kukumbuka kwamba kabla ya kulala inatakiwa kuosha uso ili kuiondosha. Hivyo hongera kwa kutoa ukumbusho.
 
Kujipenda na kujithamini ni jambo muhimu sana kwa binadamu yoyote yule. Kama hujipendi na kujithamini mwenyewe hata kumpenda na kumthamini binadamu mwenzio huwa ngumu sana.
 
Kujipenda na kujithamini ni jambo muhimu sana kwa binadamu yoyote yule. Kama hujipendi na kujithamini mwenyewe hata kumpenda na kumthamini binadamu mwenzio huwa ngumu sana.
Kabisa mkuu
 
Reactions: BAK
Kama huwez kujipenda
Na kujithamin mwenywe
Hakuna atakae kupenda
Wala kukuthamin
 
Mi napenda sana usafi hadi nimepitiliza,nashukuru umeweka uzi huu wa kuwakumbusha watu wafanye usafi kwa kiasi.
 
Tunajikimu la kufundisha watoto usafi chini ya miaka mitano kumfundisha kusafisha memo yake ingawa mwisho unamsaidia lakini mwanzo unamwacha asafishe kwanza na pia kuwafundisha Luna wa mikono lwa maji na sabuni kabla ya kula, wakitoka haja, pia baada ya kucheka navwanyama kama mnaweza, paka, ngo'mbe mbuzi nk
 
Last paragraph is much sound . Hope the message sent.
 
Hiyo nimefundishwa toka nipo chekechea nakua huku nakumbushwa so ni vigum kusahau ikiambatana na kuosha uchi pia
Ehee jamani hivi mnajitiaga madole au inakuaje. Duh mambo aya yanataka ujasiri kwani hapa tunaongelea utamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…