Kutokana na mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali uliobainiwa na serikali sikivu na inayojali watu ya Mwalimu mnamo miaka ya 1973, azimio la Arusha lilikusudia kuweka tume ya udhibiti bei "THE NATIONAL PRICE COMMISION IN TANZNIA" Kudhibiti mfumko wa bei, wakati huo Dola moja ya Marekani ilikuwa ni sawa na TSH 5/=. Tume hii ilikuwa na kazi moja ya kuchunguza kwa umakini wa kiuchumi na kuweka bei halali kwa kila bidhaa halali (fixing ceiling prices for essential items)
Kwa kawaida bei huwa inatengenezwa kwa kuzingatia gharama halisi. Mfano kama gharama ya kuzalisha umeme unit 1 (kuanzia kufua na kuusafisha na gharama zote) labda ni TSH 75/= basi bei inapatika kwa kuchukuwa TSH75+Faida (labda 25%) = TSH 93.75 ni hiyo ndiyo bei halisi inayotakiwa sokoni (market price)
Na kipao mbele kinawekwa kwa bidhaa muhimu (public good) ambazo yaipasa serikali kuhakikisha zinapatikana kwa gharama nafuu iwezekanavyo. Sifa kubwa ya public good ni kwamba 1. Non-rivary ( haishindaniwi) 2. Non excludability (haitolewi kwa ubaguzi) mfano UMEME, MAJI, HUDUMA ZA AFYA, ELIMU nk. Kuhakikisha bidhaa hizi muhimu wananchi wanapozitumia hawapata mzigo (dont feel the burden)
HALI ILIVYO
Gharama za afya, umeme, maji, elimu ni maumivu makali kwa watu wenye kipato cha chini. Hata mbadala wa umeme mafuta ya taa nayo maumivu
Gharama za chakula duni (inferior goods) mfano daghaa kwa watu wanyonge sasa ni kama anasa.
Bei ya mazao shambani anayouza mkulima ni ndogo ukilinganisha bei ya soko/madalali maumivu kwa wakulima
Bei za nauli zimeongezwa bila hata bargaining/kujadiliwa kila taasisi EWURA, SUMATRA n.k wanapanga bei kwa waonavyo wao
Shule za kata unaanbiwa gharama ni TSH 40,000 lakini mnalipishwa majengo, ulinzi hadi inafikia TSH 200,000 na zaidi. Na shule za binafsi na vyuo ndiyo maumivu makali na serikala haijali
UZALISHAJI
Asilimia kubwa ya bidhaa zilizopo sokoni ni za Kenya na Uchina, Tanzania viwanda vimekufa, hakuna udhibiti wa kuagiza bidhaa. Nchini Ghana ili uagize kitu nje lazima kiwa hakipatikani ndani
Vijana wetu hawana kazi lakini wageni wachina, wakenya nk. Wamejaa hadi kwenye kazi za ufagiaji, ofisini usisema. Managers ni aidha mzungu, mkenya au mhindi.
MASWALI
Je tume ya udhibiti wa bei kwa nini haipo leo hii, ni je ina umuhimu wowote?
Serikiali haioni haya au imeyafumbia macho.
Je katiba mpya itaweza kujibu hayo maswali au tumekazana tuu na muungano..