Umuhimu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Asasi (CSO) Kwenye Utafutaji wa Rasilimali

Umuhimu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Asasi (CSO) Kwenye Utafutaji wa Rasilimali

Joined
Feb 5, 2022
Posts
38
Reaction score
60
IDP-commences-student-placement-operations-in-Nigeria-copy-e1645028806954-860x375.jpg


Umuhimu wa Bodi ya Wakurugenzi yaani "Board of Directors" kwa Asasi za Kiraia umeanza kuonekana na kuchukuliwa kwa uzito wa kipekee. Bodi ya wakurugenzi inatoa dira ya namna ambavyo Asasi inapaswa kufanya shughuli zake, hivyo kuchochea ustawi na maendeleo ya Asasi kiujumla.
Bodi ya Wakurugenzi ya Asasi za Kiraia, kwa majina mengine inajulikana kama " Steering Committee" au " Advisory Group"
Majukumu ya Bodi
  • Kuandaa sera na mikakati kwa ajili ya Asasi
  • Kuandaa taratibu na miongozo ya kiutendaji kwa Asasi
  • Kuhakikisha Asasi inapata rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa programu.
  • Kuiwakilisha Asasi kwa wadau na majukwaa mablimbali ( It represents an organization in various constituencies)
Wajumbe wa Bodi
Kila nchi ina utaratibu wake juu ya nani na nani na kwa idadi ipi wanapaswa kuwapo kwenye chombo hiki. Kwa asasi nyingi za Kitanzania, chombo hiki kinaundwa na wajumbe 8 ambapo, 5 hutokana na waanzilishi wa Asasi na wanaobaki huchaguliwa kutokana na matakwa ya Asasi.

Ushiriki wa Bodi ya Wakurugenzi kwenye Utafutaji wa Rasilimali
Miongoni mwa majukumu makubwa ya chombo hiki, nikuhakikisha kwamba Asasi inapata rasilimali muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa program mbalimbali. Hivyo wajumbe wa chombo hiki lazima wawe na ufahamu juu ya nini maana ya "fundraising". Ushiriki wa chombo hiki katika utafutaji wa rasilimali kwa ajili ya Asasi unaweza kufanyika katika mazingira yafuatayo;
  • Mara nyingi uandaaji wa michanganuo ya miradi yaani "grant proposals" kwenye Asasi hufanywa na Fundraising Staff Team au Development/Resource and Acquisition Officer, haya majina ya vyeo hutegemeana na muundo wa uongozi wa Asasi. Lakini ninachotaka kusema hapa, ni kwamba; lazima kuwe na ukaribu na ushirikiano baina ya waandaaji wa michanguo ya miradi na bodi ya wakurugenzi. Kwa muktadha huu, jukumu la wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ni kuitambulisha Asasi kwa watendaji wa Taasisi za Ufadhili (funding Agencies) kwa ajili ya mchakato wa uombaji wa fedha kwa ajili ya Mradi husika. Na hii ndio sababu ya kupenda kuzishauri Asasi za Kiraia kuwa na wajumbe wa bodi wenye mtaji mkubwa wa rasilimali watu (social capita) au "network"
  • Wajumbe wa bodi wa Bodi hawapaswi tu kuishia kwenye "networking role" pia wanapaswa kuwa wa kwanza katika kuchangia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi kabla ya kuwafuata wafadhili wengine, kwa maana nyingine nikwamba wajumbe wa bodi wanapaswa kuwa wafadhili wa ndani wa Asasi.
  • Utoaji wa huduma muhimu kwa ajili ya Asasi. Kwa mfano; miongoni mwa wajumbe wa Asasi anaweza kuwa anamiliki ukumbi wa mikutano; hivyo kunapohitajika ukumbi kwa ajili ya kuendeshea shughuli za Taasisi, ni jukumu la Mjumbe huyu kuisaidia Asasi kupata huduma hi ya ukumbi.
  • Wajumbe/mjumbe wa bodi anapaswa kuwa anashiriki mikutano mbalimbali yenye kuwakutanisha wadau mablimbali. Kupitia mikutano hii, wafadhili wapya wanaweza kusajiliwa, na fursa mbalimbali kuweza kupatikana.
Ahsante
OMAR MSONGA (BA. PPM &CD)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
Back
Top Bottom