Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Chumvi ilikuwa na thamani kubwa sana katika utawala wa Warumi. Hakukua na umeme hivyo chumvi ilitumika kuhifadhia vyakula kama nyama na samaki. Kwa watu wa Pwani mnafahamu papa na ng’onda huu ni mfano wa vyakula vilivyo hifadhiwa na vilidumu kwa muda mrefu.
Chumvi iliitwa dhahabu nyeupe na ilitumika kulipia mishahara ya Askari. Neno salary limetokana na neno salarium kutoka katika lugha ya Latin ikimaanisha chumvi.
Warumi hawakuwa na umeme lakini walijenga majengo imara, barabara na madaraja. Siku yao ilianza saa 12 alfajiri. Walitumia vizuri mwanga wa mchana kufanya shughuli zao nyingi.
Kifungua kinywa ilikuwa ni glass ya maji, mchana wanaume walibeba mkate na cheese kula kazini. Siku ya kazi ikiisha saa nane mchana na walienda kuoga. Jioni ilikuwa ni sehemu muhimu kwao kwani walipumzika. Walicheza michezo wanayoipenda, walifanya mazungumzo ya biashara na pia walikula chakula cha jioni.
Chakula cha jioni kwa Warumi kilikuwa muhimu sana, walikaribisha marafiki na chakula kilikuwa na sehemu tatu. Wine na matunda ilikuw ni lazima kuwepo mezani. Hakukua na vijiko, umma na visu, walikula kwa mikono lakini walinawa mikono kabla na baada ya kula kila sehemu ya chakula.