Meneja CoLtd
Senior Member
- Mar 6, 2021
- 122
- 143
Utangulizi
Umaskini ni moja kati ya matatizo yanayofanyiwa utafiti sana duniani, kwa ujumla Umaskini ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile chakula, maji salama, sehemu nzuri ya kulala, huduma za afya na mavazi kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua. Hii pia inajulikana kama umaskini uliokithiri au ufukara.
Tanzania ni moja kati ya nchi yenye tatizo hili sugu la umasikini kabla na hata baada ya ukoloni, nahii inatokana na kutokuwepo mipango thabiti na endelevu ya kulidhibiti janga hili, kwani vijana wengi wanashindwa kuziendea fursa za kibiashara kutokana na uchache wa elimu ya biashara, fedha na ujasiriyamali.
Ujasiriamali ni mchakato wa utambuzi na utumiaji mzuri wa rasilimali zilizopo kutatua matatizo katika jamii kwa kuanzisha, kuendeleza na kupanua biashara mpya au biashara ya zamani.
Ujasiriyamali unajumuisha uzaalishaji, ununuzi na uuzaji wa bidhaa unaofanywa kwa malengo ya kupata faida kwa kutosheleza mahitaji ya mwanadamu na kutatua changamoto zao, mfano uuzaji wa barakoa kipindi cha uviko 19 kilisaidia kupunguza usambaaji wa ugongwa katika jamii, napia uuzaji wa barakoa ulikua ni fursa kwa jamii.
JINSI YA KUTENGENEZA WAZO ZURI LA BIASHARA
Wazo la biashara ubuniwa kwa kutafakari juu ya vitu vyote vinavyotuzunguuka, baadhi ya mawazo ya kibiasha huja kwa kusoma hali ya soko husika, kuangalia mwenendo wa dunia (trends) au kusikiliza matatizo na malalamiko ya wateja wa bidhaa au huduma fulani.
Muhimu: Mjasiriyamali lazima ajiulize maswali matatu mhimu kabla ya kuchagua wazo la biashara;
01. Je, ninauzoefu au naiweza kuifanya biashara hii?
02. Je, biashara hii italeta upinzani na kudumu kwa muda mrefu sokoni?
03. Na je, watu watakua tayari kuilipia bidhaa au huduma itokanayo na biashara hii?
VIUNGO MUHIMU VYA KUZINGATIA ILI BIASHARA IFANIKIWE
1.Wazo zuri la biashara (great business idea)
Mjasiriyamali anaweza kuwa na mawazo mengi ya biashara kwa wakati mmoja kama waya zilizofungana fungana, lakini anatakiwa achague wazo zuri na bora ambalo anaweza kulifanya kwa ufasaha zaidi na kuleta tija kwa jamii, hapa mjasiriyamali anatakiwa aangalie madhaifu yake ili asije kuchagua wazo ambalo atalishindwa.
2. Msukumo (Motivation)
Kabla ya kuanzisha biashara lazima kuwe kuna kitu kinachomsukuma mfanyaji kuifanya biashara hiyo, nahuo msukumu inabidi uweupo ndani ya moyo wa mfanyaji kiasi kwamba ataweza kuendelea kufanya biashara hiyo hata changamoto gani itokee. Msukumo unaweza kua Kijipatia kipato, sifa au kutatua changamoto za jamii.
3. Uwezo (Ability)
Mjasiriyamali anapaswa kuliendea wazo la biashara ambalo anaujuzi au uzoefu nalo ili aweze kulifanya kwa ufasaha zaidi. Nivizuri mjasiriyamali kujiuliza “MIMI NAWEZA KUFANYA NINI?” Hapa yatakuja majibu ya kazi ambazo anaweza kuzifanya kutokana na ujuzi au uzoefu alionao mfano, pale inapotokea changamoto ya upungufu wa maji kijijini, basi yule mwenye ujuzi na uzoefu wa ufundi bomba na uchimbaji wa visima hii fursa itamfaa.
4. Rasilimali (Resources)
Hapa tunajumuisha mambo yote yanayohitajika ili kufanikisha uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma, rasilimali watu, taarifa na fedha zitakazo hitajika inabidi ziwetayari na gharama zote za uzalishaji inabidi ziorodheshwe pamoja na matarajio ya fedha ambayo Mjasiriyamali atayapata kwa kuuza bidhaa au kutoa huduma husika.
WAPI MJASIRIYAMALI ATAPATA MTAJI WA BIASHARA?
1. Mfuko wa serikali (Government Fund)
Serikali ya Tanzania imekua ikifadhili, kutoa misaada na kuwakopesha fedha wananchi wake kupitia vyanzo mbalimbali kama mfuko wa halmashauri ambao serikali imeweka asilimia 10 za kuwakopesha wananchi (4% kwa vijana, 4% kwa wanawake na 2% kwa walemavu)
2. Taasisi za serikali na binafsi kama SIDO, SMIDA, NSSF, ZSSF na PSSF zimekua zikifanya kazi kubwa ya kuwawezesha vijana kuyafikia malengo yao kwa kuwafadhili na kuwapa mikopo ya biashara.
Mfano halisi ni SIDO ina mifuko miwili ya utoaji wa Mikopo. Mfuko wa Taifa wa Kuendeleza Wajasiriamali (NEDF) na Mfuko wa Mzunguko wa Mkoa (RRF) kwa mtu mmoja mmoja na kwa vikundi.
3. Tasisi zinazotoa mikopo midogo midogo (micro financial institutions), vyama vya ushirika (credit union), benki za kibiashara kama NBC, NMB, CRDB na nyengine nyingi zimekua zikitoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambao wamekidhi vigezo na masharti ya kupata mikopo.
Zingatio:
"Kopa kwenye taasisi yenye leseni ya Benki Kuu ya Tanzania kuepuka usumbufu. Zingatia malengo ya mkopo, elewa mkataba na ubaki na nakala iliyosainiwa." (BOT)
UTUNZAJI FEDHA NA UWEKEZAJI
Changamoto kubwa ya watanzania ni kutofahamu matumizi mbadala ya fedha ukiachilia mbali matumizi ya kila siku ya kununua chakula na kuweka pesa kwaajili ya dharura kama kuumwa pia pesa inatakiwa ewekezwa kwenye taasisi mbalimbali za fedha ili kupata faida zaidi.
Mfano mtu anayepata 100,000 Tzs kwa mwezi anaweza kuwekeza 1,200,000 Tzs kwa mwaka kwenye taasisi ya fedha au benki inayotoa riba ya 3% na akapata faida ya 36,000.
Na kwa wale ambao hawataki riba, basi wanaweza kuwekeza faida wanayopata kwenye biashara au miradi mingine ili wapate faida zaidi.
HITIMISHO
Serikali ya Tanzania inapaswa kuongeza juhudi za utoaji wa Elimu ya Ujasiriyamali, Biashara na Fedha kwa watanzania hasa vijana na wanafunzi kama elimu mbadala, maana masomo mengi ya mashuleni kama fizikia, bailojia, uraia, historia na mengine mengi huwaandaa vijana kuwa tegemezi.

Upvote
5