SoC03 Umuhimu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa na Tovuti yake Itayosaidia Utoaji na Upatikanaji wa Taarifa kwa ulinzi wa Taifa letu

Stories of Change - 2023 Competition

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS) Ni Idara ambayo inamajukumu ya kukusanya, kuchunguza na kuchambua Taarifa na shughuli zote zinazohusiana na Usalama wa Taifa. Ikiwa ni pamoja na kubaini matishio yote dhidi ya Tanzania lakini pia kushauri wizara zote juu maswala ya ulinzi na Usalama, Hivyo Tunaweza kusema idara hii ni idara ya muhimu na ya msingi katika uhai wa nchi yetu.

Katika kutekeleza majukumu yake idara inatumia mifumo na njia mbalimbali, Tufahamu yakuwa tupo katika dunia ya mabadiliko makubwa, Hivyo ni muhimu kwa idara yetu ya usalama wa taifa kuwa na mfumo wa kidigitali yaani tovuti ambayo raia wanaweza ingia na kuona taarifa mbalimbali lakini pia kuwezesha raia kutoa taarifa mbalimbali zitakazo saidia idara katika ufanyaji kazi.

Faida zitakazo tokana na uwepo wa tovuti hii sii tu wananchi kupata taarifa kutoka kwa idara bali pia idara kupokea taarifa kutoka kwa wananchi. Tukumbuke kuwa usalama wa Taifa unaanza na mwananchi, Hivyo ni muhimu kwa idara kuwa na mfumo utakao unganisha na kukuza mahusiano ya moja kwa moja na wananchi kwa kufanya hivi tutakuwa tumewavuta karibu wananchi na hivyo kuwa na mfumo shirikishi kati ya serikali na wananchi

MUUNDO WA TOVUTI

Napendekeza mfumo wa tovuti hii uwe na sehemu zifuatazo:-

SEHEMU YA HISTORIA YA IDARA

Katika sehemu hii idara iweke historia yake toka kuanzishwa kwake lakini pia viongozi waliowahi kuhudumu katika nafasi za ukurugenzi wa idara na historia zao, Lakini pia maono ya idara pamoja Na dira yake yaelezwe Kwa ufupi.

SEHEMU YA TAARIFA KUTOKA IDARA.

Sehemu hii iwe ni sehemu ambayo mwananchi akiingia ataona taarifa mbalimbali kama tahadhari za nchi zenye machafuko na nchi ambazo zina matishio ya ugaidi taarifa hizi idara itapokea kutoka kwa mabalozi wa Tanzania walio katika nchi mbalimbali na mara moja idara itaweka taarifa hizo katika tovuti yake hii itasaidia Wafanyabiashara, Watalii pamoja na Wanafunzi katika kupanga ratiba zao.

SEHEMU YA TAKWIMU.

Sehemu hii iwe na takwimu mbalimbali za Tanzania lakini pia takwimu za nchi nyingine za kijiografia, Kisiasa, Kiuchumi, biashara zinazofanywa na nchi nyingine. Mfano Mtanzania akitaka kujua ni maeneo gani katika nchi ya Rwanda biashara ya kuuza vitunguu ni kubwa moja kwa moja anaweza pata taarifa hizo kwenye tovuti ya usalama wa taifa taarifa za kweli na zenye uhakika.

SEHEMU YA NUKUU, VIPEPERUSHI NA MAKALA.

Hapa kuwekwe nukuu mbalimbali za viongozi wa nchi pamoja na nukuu za wakurugenzi wa idara ambazo zinahusiana na maswala ya ulinzi na usalama lakini pia vipeperushi na Makala ambazo zitakuwa zinaelezea umuhimu wa wananchi kushiriki na kutoa michango itayosaidia ukuaji mzuri wa nchi yetu, Makala za uelimishaji juu ya hatari za Rushwa, Ufisadi na ugaidi.

SEHEMU YA WANACHI KUTOA TAARIFA

Hii ni sehemu ya muhimu kwani hapa idara inaweza kukusanya taarifa mbalimbali za kiusalama kupitia wananchi sehemu itaruhusu wananchi kutoa taarifa ambapo mwanachi akiingia mfumo utamlinda na Hivyo kutoa taarifa zinazohusu ugaidi lakini pia kutoa taarifa juu ya viashiria vyovyote ambavyo ni hatari kwa taifa Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na Kidini.

Tukumbuke kuwa idara ina jukumu nzito la kuilinda Tanzania dhidi ya matishio ya aina yeyeto Hivyo basi suala la kuwahusisha wananchi juu ya ulinzi na usalama kwa nchi yao si suala la kupuuzwa.

FAIDA ZA MFUMO KWA UJUMLA

  • Kutoa nafasi ya wananchi kushiriki katika ulinzi na usalama wa nchi yao Hivyo kujenga mahusiano mazuri baina ya serikali na wananchi.
  • Wananchi kujua historia ya nchi yao lakini pia kupata nafasi ya kujifunza maswala mbalailmbali na kwa kufanya hivi idara itakuwa inakuza na kufundisha uzalendo kwa wananchi hali hii itasaidia kuondoa Ukabila, Udini na Ukanda kwani tutategema idara kupitia tovuti yake kuweza kukemea na kuelimisha jamii. Hii itasaidia sio tu mahusiano ya wananchi na serikali lakini pia itaudumisha uhusiano huo.
  • Idara kuwa na wingi wa taarifa kutoka kila kona ya Tanzania na Hivyo kuifanya idara kuwa na utajiri wa taarifa ambazo idara itazitumia katika kutekeleza majukumu yake.


CHANGAMOTO ZA MFUMO

  • Ufikshwaji wa Taarifa za uongo, Watu wenye nia ovu wanaweza tumia tovuti kufikisha taarifa za uongo kwa idara jambo ambalo litaleta usumbufu kwa idara.
  • Kudukuliwa kwa mfumo, Hii ni dunia ya utandawazi watu wenye nia ovu wanaweza dukua mfumo na kupata taarifa ambazo wananchi wamezitoa kwa idara.
NJIA ZA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO HIZO

Njia nzuri ya kupambana na changamoto hizo kwanza ni kuundwa kwa tovuti yenye ulinzi na usalama wa hali ya juu ambao utakuwa na uwezo mkubwa wa kubaini na kuzuia shambulio lolote la kujaribu kudukua mfumo lakini pia pale ambapo mwananchi anataka kutoa taarifa mfumo utamtaka ajaze taarifa zake binafsi na aruhusu mfumo kuweza kufikia taarifa zake za chombo anachotumia kuwasiliana na idara. Hii itasaidia wananchi kuogopa kutoa taarifa za uongo hivyo kuondoa usumbufu kwa idara,

Pia kuundwe kwa sheria ambayo endapo itabainika mwananchi ametoa taarifa za uongo kwa nia ovu ya kusumbua serikali hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

HITIMISHO

Tunatambua idara inafanya kazi zake kwa usiri mkubwa, Hivyo taarifa ambazo idara itakuwa inatoa ni taarifa ambazo hazina madhara dhidi ya usalama wa Tanzania. Pia nashauri idrara kupitia upya mifumo yao ya kuajiri na kuboresha idara ili iakisi dunia ya sasa.
 
Upvote 15
Kama una taarifa za kiharifu pereka polisi, icho ulichotaka kiwe humu kiende polisi, wao wanajua namna ya kufanyia kazi. Kama maboresho basi yakafNyiks polisi mana wao ndio wenye jukumu la kuchukua raw news kutoka kwa wananchi. baada ya hapo ndio watajua vyombo vingine vihusike vipi kwa uzito wa tatizo, kuna jwtz kama jambo linawahusu watahusika au Tiss wenyewe ipo ivyo
 
TISS kuchukua taarifa kutoka polisi ni njia moja wapo ya wao kupata taarifa lakini sio njia hiyo tu inabidi itumike, Kwani njia za upatikanaji taarifa ni nyingi kwa kuwa lengo ni kulinda maslahi ya nchi ni lazima kuwa na njia nyingi na moja wapo ni hili ya kupitia tovuti.
Kumbuka kuwa sio watu wote wanaweza kwenda kutoa taarifa polisi ntakupa mfano mtu ana RB labla ameripotiwa kauza mali kimakosa au kajeruhi mtu polisi wana mtafuta lakini katika kukimbia kimbia mtu huyu akapata taarifa nyeti kuhusu ugaidi vipi mtu huyu ataenda kutoa taarifa polisi wakati polisi wanamtafuta kwa kosa la kujeruhi au kuiba au kosa lolote tu. Huoni kuwa kwa kutegemea chanzo kimoja cha taarifa utakuwa umekosa taarifa muhimu .?
 
Umeeleza vizuri sana, Ndio maana utaona Hapa kwetu usalama wa taifa upo chini ya rais badala ya rais kuwa chini ya usalama wa taifa.
 
Ambacho hatuelewani hapa ni kitu kimoja tu,muandishi wa makala hana maana kwamba TISS wawe na website ambayo wataweka taarifa zao za kiinteligensia,hapana.

Taarifa za kiupelelezi ni siri na itabaki kuwa ni siri kamwe haziwezi wekwa hazarani.

Lengo lamuandishi ni kwamba TISS wawe na website ambayo itawawezesha watanzania wote kuwafikia kwaurahisi,ni kuwapatia taarifa za msingi pale inapohitajika,ili kusaidia kulinda hata usalama wa watoa taarifa.

Na hili wao sio wa mwanzo,Jeshi la Polisi,JWTZ na vyombo vyengine vyote vina website kwani ndo kusema taarifa zao za ndani zimevuja kwa kuwa na hizo website au!!
 
Mkuu hebu twende taratibu mfano wa taarifa unayoweza kuitoa Tiss ni ipi nitajie
 
Kwa hii idara ilivyojipanua kila sehemu ofisi, kijiweni, shuleni ,masokoni ,na sehemu mbali mbali hadi vijijini huko wapo haina haja ya kufanya unavyofikiria wewe
Na ndio maana taarifa kabla hujaitoa wao washaijui siku nyingi
SIO KWELI!!!

kama kuna chombo ambacho hakikupaswa kuwa na website basi ni JWTZ,mana ndio chombo pekee ambacho majukumu yake hayahusiani na mambo ya ndani,lakini wana web na jamii inawafikia pale inapohitajika.

Hichi kisingizio cha usiri ni outer cover tu ya kuficha maovu yanayotendeka huko nyuma ya pazia na kulinda maslahi binafsi ya watu.

Nasi hatutapaacha bure tu kwa kuwa fedha zinazotumika kuendesha taasisi hii ni kodi ya wananchi hivyo ni lazima ilinde na iheshimu maslahi ya taifa.
 
Atatoa polisi mtandaoa, amba watatengeza kama utakavyo iwe Tiss, mfano hapa jamii forum kunaweza kuwa na uzi wa riport polisi, na Tiss watachungulia humo humo bila kujulikana. Ni jambo la kusuka mfumo.
 
Yaani kama ulikuwa kwenye akili yangu. Asante kwa kutoa elimu umeeleza kwa lugha rahisi sana mwenye kuelewa na aelewe.
 
Ukiangalia mwisho wa hii posti kuna kialama kimewekwa ^ bonyeza hapo mkuu utakuwa tayari umepigia kura bandiko hili asante
 
Mkuu hebu twende taratibu mfano wa taarifa unayoweza kuitoa Tiss ni ipi nitajie
1-Historia ya TISS
2-Dhamira na Malengo ya TISS
3-Mifumo ya Ajira
4-Bajeti yake
5-Viongozi wa juu wa TISS na uteuzi wao,kwa wale ambao kujulikana kwa madaraka yao hakutaathiri utendaji wa taasisi.
5-Utoaji wa elimu ya usalama wa Taifa kwa umma kupitia machapisho mbalimbali yasiokuwa na siri za nchi.
6-Mawasiliano
7-Nafasi za ajira

Hayo ni baadhi tu,yapo mengi,xx iambie ni lipi kati ya hayo niliokutajia linaweza kusababisha kuvuja kwa siri za ndani ta taasisi km mnavyodai.

Nasisitiza tena TISS ni taasis ya umma km zilivyo taasisi nyengine,isigeuzwe kuwa kichaka cha watu fulani kwa maslahi yao.

Kuna koo nchi hii tangu uhuru wanarithishana hii kazi,unakuta karibu ukoo mzima wapo Tiss kwa sababu tu mfu.o wa uajiti wameushikilia wao,umma hauhusishwi,wanarithisha watoto wao tu,hii ni xawa kweli??

Kisingizio kikubwa ni siri,xx hata ajira nayo ni siri??hata bajeti ni siri?hata mawasiliano ni siri?
Hata viongozi wa juu ni siri??

Hebu tuache ubabaishaji basi,,huu ulimwengu wa utandawazi,tunajifunza mengi toka kwa wenzetu ndo mana hatutaki kuendelea kuburuzwa.
 
Sawa, mm binafsi nimekuelewa
 
Ukiangalia mwisho wa hii posti kuna kialama kimewekwa ^ bonyeza hapo mkuu utakuwa tayari umepigia kura bandiko hili asante
Nimebonyeza wameniambia nimesubscribe,sijui kama hiyo ndo kura au vp!!!
 
Mwisho kabisa,maana nivuke mpaka izi comment au??
Hapana mwisho wa uzi kabla haujaanza comment ya kwanza
Nimebonyeza wameniambia nimesubscribe,sijui kama hiyo ndo kura au vp!!!
Sio hapo mkuu, angalia sehemu imeandikwa vote alafu kuna kialama cha ^
Kama inakuwa ngumu kukiona jaribu kuufungua huu uzi upya kabla hujaingia ndani kusoma utaona sehemu ya vote njia ya pili ni ufungue kabisa uzi mwisho wa huu uzi kabla ya comment ya kwanza kuna sehemu ya report, like hapo pia kuna sehemu ya vote bonyeza hapo utakuwa umepiga kura.
Kwa maelezo zaidi ingia kwenye jukwaa la stories of change utaona jf wameeleza kwa undani jinsi ya kupiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…