SoC03 Umuhimu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa na Tovuti yake Itayosaidia Utoaji na Upatikanaji wa Taarifa kwa ulinzi wa Taifa letu

Stories of Change - 2023 Competition

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS) Ni Idara ambayo inamajukumu ya kukusanya, kuchunguza na kuchambua Taarifa na shughuli zote zinazohusiana na Usalama wa Taifa. Ikiwa ni pamoja na kubaini matishio yote dhidi ya Tanzania lakini pia kushauri wizara zote juu maswala ya ulinzi na Usalama, Hivyo Tunaweza kusema idara hii ni idara ya muhimu na ya msingi katika uhai wa nchi yetu.

Katika kutekeleza majukumu yake idara inatumia mifumo na njia mbalimbali, Tufahamu yakuwa tupo katika dunia ya mabadiliko makubwa, Hivyo ni muhimu kwa idara yetu ya usalama wa taifa kuwa na mfumo wa kidigitali yaani tovuti ambayo raia wanaweza ingia na kuona taarifa mbalimbali lakini pia kuwezesha raia kutoa taarifa mbalimbali zitakazo saidia idara katika ufanyaji kazi.

Faida zitakazo tokana na uwepo wa tovuti hii sii tu wananchi kupata taarifa kutoka kwa idara bali pia idara kupokea taarifa kutoka kwa wananchi. Tukumbuke kuwa usalama wa Taifa unaanza na mwananchi, Hivyo ni muhimu kwa idara kuwa na mfumo utakao unganisha na kukuza mahusiano ya moja kwa moja na wananchi kwa kufanya hivi tutakuwa tumewavuta karibu wananchi na hivyo kuwa na mfumo shirikishi kati ya serikali na wananchi

MUUNDO WA TOVUTI

Napendekeza mfumo wa tovuti hii uwe na sehemu zifuatazo:-

SEHEMU YA HISTORIA YA IDARA

Katika sehemu hii idara iweke historia yake toka kuanzishwa kwake lakini pia viongozi waliowahi kuhudumu katika nafasi za ukurugenzi wa idara na historia zao, Lakini pia maono ya idara pamoja Na dira yake yaelezwe Kwa ufupi.

SEHEMU YA TAARIFA KUTOKA IDARA.

Sehemu hii iwe ni sehemu ambayo mwananchi akiingia ataona taarifa mbalimbali kama tahadhari za nchi zenye machafuko na nchi ambazo zina matishio ya ugaidi taarifa hizi idara itapokea kutoka kwa mabalozi wa Tanzania walio katika nchi mbalimbali na mara moja idara itaweka taarifa hizo katika tovuti yake hii itasaidia Wafanyabiashara, Watalii pamoja na Wanafunzi katika kupanga ratiba zao.

SEHEMU YA TAKWIMU.

Sehemu hii iwe na takwimu mbalimbali za Tanzania lakini pia takwimu za nchi nyingine za kijiografia, Kisiasa, Kiuchumi, biashara zinazofanywa na nchi nyingine. Mfano Mtanzania akitaka kujua ni maeneo gani katika nchi ya Rwanda biashara ya kuuza vitunguu ni kubwa moja kwa moja anaweza pata taarifa hizo kwenye tovuti ya usalama wa taifa taarifa za kweli na zenye uhakika.

SEHEMU YA NUKUU, VIPEPERUSHI NA MAKALA.

Hapa kuwekwe nukuu mbalimbali za viongozi wa nchi pamoja na nukuu za wakurugenzi wa idara ambazo zinahusiana na maswala ya ulinzi na usalama lakini pia vipeperushi na Makala ambazo zitakuwa zinaelezea umuhimu wa wananchi kushiriki na kutoa michango itayosaidia ukuaji mzuri wa nchi yetu, Makala za uelimishaji juu ya hatari za Rushwa, Ufisadi na ugaidi.

SEHEMU YA WANACHI KUTOA TAARIFA

Hii ni sehemu ya muhimu kwani hapa idara inaweza kukusanya taarifa mbalimbali za kiusalama kupitia wananchi sehemu itaruhusu wananchi kutoa taarifa ambapo mwanachi akiingia mfumo utamlinda na Hivyo kutoa taarifa zinazohusu ugaidi lakini pia kutoa taarifa juu ya viashiria vyovyote ambavyo ni hatari kwa taifa Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na Kidini.

Tukumbuke kuwa idara ina jukumu nzito la kuilinda Tanzania dhidi ya matishio ya aina yeyeto Hivyo basi suala la kuwahusisha wananchi juu ya ulinzi na usalama kwa nchi yao si suala la kupuuzwa.

FAIDA ZA MFUMO KWA UJUMLA

  • Kutoa nafasi ya wananchi kushiriki katika ulinzi na usalama wa nchi yao Hivyo kujenga mahusiano mazuri baina ya serikali na wananchi.
  • Wananchi kujua historia ya nchi yao lakini pia kupata nafasi ya kujifunza maswala mbalailmbali na kwa kufanya hivi idara itakuwa inakuza na kufundisha uzalendo kwa wananchi hali hii itasaidia kuondoa Ukabila, Udini na Ukanda kwani tutategema idara kupitia tovuti yake kuweza kukemea na kuelimisha jamii. Hii itasaidia sio tu mahusiano ya wananchi na serikali lakini pia itaudumisha uhusiano huo.
  • Idara kuwa na wingi wa taarifa kutoka kila kona ya Tanzania na Hivyo kuifanya idara kuwa na utajiri wa taarifa ambazo idara itazitumia katika kutekeleza majukumu yake.


CHANGAMOTO ZA MFUMO

  • Ufikshwaji wa Taarifa za uongo, Watu wenye nia ovu wanaweza tumia tovuti kufikisha taarifa za uongo kwa idara jambo ambalo litaleta usumbufu kwa idara.
  • Kudukuliwa kwa mfumo, Hii ni dunia ya utandawazi watu wenye nia ovu wanaweza dukua mfumo na kupata taarifa ambazo wananchi wamezitoa kwa idara.
NJIA ZA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO HIZO

Njia nzuri ya kupambana na changamoto hizo kwanza ni kuundwa kwa tovuti yenye ulinzi na usalama wa hali ya juu ambao utakuwa na uwezo mkubwa wa kubaini na kuzuia shambulio lolote la kujaribu kudukua mfumo lakini pia pale ambapo mwananchi anataka kutoa taarifa mfumo utamtaka ajaze taarifa zake binafsi na aruhusu mfumo kuweza kufikia taarifa zake za chombo anachotumia kuwasiliana na idara. Hii itasaidia wananchi kuogopa kutoa taarifa za uongo hivyo kuondoa usumbufu kwa idara,

Pia kuundwe kwa sheria ambayo endapo itabainika mwananchi ametoa taarifa za uongo kwa nia ovu ya kusumbua serikali hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

HITIMISHO

Tunatambua idara inafanya kazi zake kwa usiri mkubwa, Hivyo taarifa ambazo idara itakuwa inatoa ni taarifa ambazo hazina madhara dhidi ya usalama wa Tanzania. Pia nashauri idrara kupitia upya mifumo yao ya kuajiri na kuboresha idara ili iakisi dunia ya sasa.
 
Upvote 15
Kuwepo kwa tovuti ya TISS hakuta saidia kitu ukizingatia kwamba maelezo yatakayowekwa kwenye hiyo tovuti yatakuwa siyo ya kweli,hawataweza kujianika kwenye tovuti,itakuwa ni geresha TU
 
Kuwepo kwa tovuti ya TISS hakuta saidia kitu ukizingatia kwamba maelezo yatakayowekwa kwenye hiyo tovuti yatakuwa siyo ya kweli,hawataweza kujianika kwenye tovuti,itakuwa ni geresha TU
Unataka kuniambia uwepo wa tovuti ya CIA Marekani haisaidii kitu chochote?
 
Geeereeeeshaaaaaaaaa..
Kumbuka tovuti haipo designed kwa ajili ya kupokea tu taarifa lakini pia kutoa taarifa.
Ndio maana ukiingia kwenye tovuti ya CIA utaona makala mbalimbali za kujifunza.
Lakini pia kupitia Tovuti ni rahisi kujua vitu ambavyo wananchi wanatakujua kuhusu TISS ambayo vinawachanganya hivyo ni rahisi kwa TISS ku set mambo yao kwa kuzingatia uhitaji wa jamii.
Tusiishie kuangalia upande mmoja tu .
 
Haisaidii Ile ni bosheni tu.
Je kuna faida ya kitu kuwa kama bosheni tu?
Mpaka wakaamua kuweka ili iwe kama bosheni that means kuna faida, Haiwezekani serikali ya Marekani iajiri watu wa kuchapisha makala katika tovuti watu wa kuisanifu tovuti n.k iwalipe then tovuti isiwe na faida yeyeto hiyo haiingii akilini.
Na kama kweli ni bosheni tu kama unavyodai basi ipo faida isiyoonekana moja kwa moja wana ipata.
 
Haisaidii Ile ni bosheni tu.
Tuje upande wa pili kwanini Taasisi nyingine tena nyeti kabisa kama jeshi ina tovuti hapahapa Tanzania JWTZ wanayo tovuti unataka kuniambia jeshi lilikosea kuwa na tovuti.
Kingine ni kuwa sio kwamba tovuti inakuwa ndio chanzo cha taarifa zote hapana, idara itakuwa inafanya kazi zake kama kawaida kwa kutumia vyanzo vyake ila tovuti inakuwa moja katika ongezeko litalochochea uwajibikaji kama haina faida kwao basi itakuwa na faida kwa wananchi usiangalie faida ya upande mmoja tu.
 
Maelezo yako ni ushauri mzuri kwa polisi .tiss haifanyi kazi hivo tiss ni level ya research sio vya sijui kijana wa halmashaur kajenga kagorofa .wao wako mambo ya uhujumu uchumi(mambo kama kuficha sukar) uhamiaji haramu(sio hivi vya mkenya kaja kula bia arusha) utakatishaji fedha kimataifa etc na asilimia 80 ya kazi yao ni ushauri kwa serikali na viongozi wengine kijamii kuvunja minyororo ya uharifu .kukusanya taarifa za kiusalama na kuzifanyia upembuzi hata kubashiri uwezekano wa kudhibiti yajayo.wewe ukiwa na ishu na mzalendo Peleka polisi quote takukulu imeisha
 
TISS wapo jeshi la polisi, uhamiaji, TAKUKURU, wapo jeshi la magereza, BOT, TRA, JWTZ, Mikoani, Wilayani, Halmashauri, Vyuoni na Taasisi nyingine za serikali na binafsi unadhani huko wanakusanya nini?
Kazi ya TISS ni kuilinda nchi dhidi ya Tishio lolote elewa neno lolote kwa Tanzania.
Neno kulinda lisikuchanganye TISS wao wanalinda kwa njia ya kuchambua, kuchunguza na kushauri maswala yote yanayohusu usalama kwa Tanzania
Sasa twende taratibu Mtu anaweza kuwa ni gaidi amefanya kazi na vikundi vya kigaidi mfano M -23 Lakini rada za usalama hazijambaini mtu huyo akatoka huko msituni kaja mtaani ni mtanzania akawa anaishi akafanya kosa labda kuiba n.k akahukumiwa miezi 6 jela, Huko jela TISS lazima wawepo ili kubaini hatari ya kila mfungwa na endapo wakabaini kuwa alishajihusisha na ugaidi ndio huyo mfungwa atatolewa magereza za kiraia na kupelekwa kuhojiwa na watu wa military intelligence huko jeshini.
Huu ni mfano mdogo tu nimekupa ni jinsi gani TISS wanavyofanya kazi ndani ya magereza ninaweza kukupa mifano ya kila Taasisi niliyokutajia ila muda ndio haunitoshi, Kwa mfano huo utaona kuwa kumbe TISS wao kazi ya kubwa ni kupata taarifa na kuzipeleka sehemu husika, Sasa swali ni vipi Taasisi inayo deal na ukusanyaji wa taarifa haina tovuti?, Japo kuwa wana vyanzo vyao vya ukusanyaji taarifa lakini pia ni vyema wakawa na tovuti.
Hivyo kauli yako ya kusema kuwa TISS haidili na mambo madogo sio kweli ina deal na mambo madogo tena sana maana kwenye mambo madogo ndipo yalipojificha mambo makubwa.
Na ukitaka kujua kuwa wanafuatilia mambo yote jiulize kwenye hayo mataasisi yote huko wanafanya nini.
 
Asante sana Mjumbe wa TEC.
Hii ni akili kubwa.
Akili ya TEC.
 
ANDIKO zuri sana.

Bahati Mbaya unataka kuchanganywa Majukumu ya POLISI na TISS.

Kila Wilaya Ina AFISA usalama WA Wilaya TISS.
Ambaye yupo JIRANI mno na TISS.

TATIZO LA hii IDARA ni uwazi Katika AJIRA
 
ANDIKO zuri sana.

Bahati Mbaya unataka kuchanganywa Majukumu ya POLISI na TISS.

Kila Wilaya Ina AFISA usalama WA Wilaya TISS.
Ambaye yupo JIRANI mno na TISS.

TATIZO LA hii IDARA ni uwazi Katika AJIRA
Inabidi wafanye uwazi katika mfumo wa ajira.
 
Asante kwa kunielimisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…