Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kuna upuuzi unafanyika nchi hii nadhani ni kuzimu tu wanaweza kuuelewa.
Tunaposema kuna haja ya kupata KATIBA MPYA kuuondoa huu upuuzi tuna maanisha kweli maana hii nchi imefikia hatua mbaya kiasi cha kusikitisha na kuogopesha.
Mkuu wa Itifaki Serikalini ( Chief of Protocol) ni cheo cha utendaji. Cheo hiki kina hadhi ya Mkurugenzi pale Wizara ya Mambo ya Nje. Mtumishi huyu analipwa mshahara kwa kodi za Wananchi wa Tanzania ambao ndani yake kuna wanachama wa vyama tofauti vya siasa. Analipwa posho kwa kodi hizo za wananchi ambazo pia kuna Watanzania ambao sio wanachama wa chama chochote cha siasa.
Mtumishi huyu anapovaa nguo za CCM tena kwenye sherehe ya CCM ni upuuzi na matusi makubwa sana juu ya utawala bora na utawala wa Sheria.
Ni kielelezo cha ujinga sio tu wake ila kwa Watanzania kuwa tupo kwenye hali mbaya sana.
Kwa kifupi mtumishi huyu hapaswi hata kuwepo kwenye shughuli ya Chama maana shughuli za chama zinapaswa kuratibiwa na kuendeshwa na Chama husika.
Mungu atusaidie.
Pichani:
Mkuu wa Itifaki Serikalini Yusuf Mndolwa akimkaribisha Waziri Mkuu ndani ya Mkutano wa CCM.