Umuhimu wa KATIBA MPYA: Mkuu wa Itifaki Serikalini avaa nguo za CCM

Hiivi wananchi wanaendaje kuhudhuria mikutano ambayo haina faida kwa nchi kama hii?
 
Mkuu wa Itifaki ni mtumishi wa serikali ambaye hana kazi yoyote katika mkutano wa CCM.

Huyo ni sawa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje tu.

Gone are the days of Ambassador Joshua Opanga.
 
Unaanza kupoteza "focus"...

Shati alilovaa si la CCM....

Si kila rangi ya kijani ni CCM....

Unataka KUANDAMANA kuifuta rangi ya kijani katika bendera yetu ya JMT?!!

#Nchi kwanza!
 
Hilo ni shati la ccm?? Ninyi nanyi acheni cheap politics.
 
Nilikua najiuliza sana huyo jamaa ni nani . Asante sana mtoa mada
 
Imeandikwa wapi kwamba ni shati la ccm au kila kijani na njano ni ccm? Mbona hujamlaumu kwamba kavaa yanga? Hilo shati halina nembo yoyote ya ccm.
 
Analazimika, kufanya kaz serukalini ni ngumu sana wewe kutenganishwa na Ccm maana utaambiwa unatekeleza ilani ya chama tawala (Ccm)
Kwa hiyo ni Tanzania tu ambapo Watumishi wa Serikali wanalazimishwa kufanya kazi za Chama kilichopo madarakani only because wanatekeleza ilani ya Chama?

Huu ni upuuzi uliotukuka.
 
Amevaa shati la kitenge, lisilo na nembo Wala Jina la CCM.
Ukisha vaa rangi za mboga mboga katika kuadhimisha siku ya Chama cha Mboga mboga na wewe ni mfuasi wa chama cha Mboga mboga.
 
Sio kila kijani ni CCM
Anafanya nini kwenye shughuli ya CCM?

Huyo ni mtumishi wa Umma na hiyo ni shughuli ya Chama. Inapaswa kuratibiwa na chama kwenye kila kitu.

Kwa tafsiri ya kawaida tu hapo kuna fungu la Serikali ambazo ni kodi za wananchi limeenda kugharamia shughuli za Chama.

Hii nchi inawezekana aliyeturoga afufuliwe maana huu upumbavu umezidi sasa!
 
Sio yule mkalimani?
 
Nadhani kama sio chuki zilizopitiliza dhidi ya CCM utakuwa na matatizo ya macho!
Nguo alizovaa huyo jamaa hazina uhusiano wowote na CCM.
Karibu kuzoom hilo shati uone kama kuna alama yoyote ya CCM.
Jambo jingine kabla ya kuleta katiba mpya ni kipengele kipi cha katiba ya Sasa kimeruhusu watumishi wa serikali kama huyu hapa kuvaa nguo za CCM.
Point yangu ni kwamba kuna uwezekano tukaweka katiba mpya na mambo yakawa hayahaya!.
 
Kabla ya kuangalia kama nguo yake ina nembo ya CCM swali la kwanza ulilopaswa kujiuliza ni huyo mtumishi wa umma anayelipwa mshahara kwa kodi za wananchi anafanya nini kwenye shughuli ya chama?
 
Mkuu wa Itifaki ni mtumishi wa serikali ambaye hana kazi yoyote katika mkutano wa CCM.

Huyo ni sawa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje tu.

Gone are the days of Ambassador Joshua Opanga.
Sasa kama rais tuu ana chama sembuse mkuu wa itifaki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…