SoC03 Umuhimu wa Katiba Mpya na Kasi ya Mabadiliko

SoC03 Umuhimu wa Katiba Mpya na Kasi ya Mabadiliko

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Sep 20, 2019
Posts
15
Reaction score
35
#Storyofchange2023
Mwandishi: Wa Kale

Mawasiliano,
Email: officialmapatotz@gmail.com
Simu: +255745922142

flyerdesign_11052023_215215.JPEG

Utangulizi: Katiba naweza kusema, ni taratibu, miongozo, kanuni na sharia zinazotumika katika utekelezaji sahihi wa majukumu mbalimbali katika maisha ya kila siku ya mwanadamu.

Ikiwa katiba inahusu maisha ya kila siku ya mwanadamu na maisha ya mwanadamu yanabadilika kila siku basi ni wazi kuwa katiba nayo inahitaji mabadiliko. Mabadiliko ya katiba yanaweza kufanywa kwa namna mbalimbali:​
  • Kuandika Katiba Mpya​
  • Kurekebisha katiba ya zamani​
  • Kuondoa Baadhi ya vipengele katika katiba​
  • Kuongeza vipengele Katika katiba.​
Mabadiliko hayo yote yanategemea zaidi mahitaji ya wananchi katika nyanja mbalimbali kama vile kiuchumi, kijamii, kisiasa, n.k.

Katika nchi zote duniani, Ikiwemo Afrika hasa Tanzania Mabadiliko ya katiba mpya hayakwepeki.

Kwa Tanzania Mabadiliko au Katiba Mpya ni muhimu kwa sababu zifuatazo:​

> Mabadiliko ya zama:
Ni wazi kuwa katiba yetu imeandikwa miaka mingi iliyopita kutoka zama za ujima, utandawazi mpaka sasa ni zama za digitali.​
Kila zama zina mahitaji yake muhimu ya kikatiba.​
Kwa nchi kama Tanzania tunahitaji sheria mpya/katiba mpya ili kudhibiti na kuboresha mifumo inayotokana na Mabadiliko hayo kwa namna zifuatazo:
  • Mabadiliko ya mifumo ya internet hasa katika suala la matumizi ya data,
  • uhuru wa kutoa maoni katika mitandao ya kijamii,
  • uhuru wa vyombo vya habari,
  • uhuru wa umiliki na matumizi ya blogu, YouTube channel, tovuti n.k
  • Uhuru wa kutumia ndege zisizo na rubani katika kuchukua Taarifa maarufu kama drones.

Ni wazi kua kwa Tanzania kuna mifumo dhaifu ya kudhibiti masuala ya internet, uhuru wa kutoa maoni na umiliki wa nyenzo za kutolea maoni, uhuru wa vyo vya habari n.k.​
Ambapo sheria zilizopo hazifikii kiwango cha mabadiliko yaliyopo kwa sasa na hivyo kuwepo kwa uhitaji wa katiba mpya.​

> Mabadiliko Ya Kiutawala:
Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kiutawala ambapo mambo yafuatayo ni muhimu :​
  • Kuondoa mamla ya kiongozi Yeyote kumfukuza kazi mtu yeyote bila amri ya mahakama kama alikua ameajiliwa au kufungia huduma yoyote iliyopo kihalali au kwa mjibu wa kanuni za kisheria.​
  • Kupunguza mamlaka ya Rais: Mamlaka aliyonayo raisi kikatiba yanatakiwa kupunguzwa ikiwemo mamlaka ya kuteua na kuunda tume ya uchaguzi, Mamlaka ya kuteua wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, Kuteua wakurugenzi n.k, Badala yake viongozi hawa wachaguliwe na wanachi au wawakilishi wa wanachi kama wenyeviti wa vijini au madiwani.​
  • Kupunguza Ukomo wa utawala / kugombea kwa Rais kutoka miaka 10 na kubaki 5 tu.​
  • Kupunguza Umri na vigezo vya kuchaguliwa kuwa Rais au Mbunge.​
  • Mgawanyo sahihi wa madaraka na utekelezaji wake, Yaani Kusiwepo kuingiliana kwa viongozi katika utekelezaji wa majukumu.​
  • Mgawanyo wa nchi katika mfumo wa majimbo; Hii itasaidia ufikiwaji wa wanachi kwa urahisi.​
  • Kuruhusu Rais kushitakiwa hata kama yupo madarakani kama ametenda kosa kisheria bila kujali ukubwa wa kosa.​
  • Kuondoa kabisa mamlaka ya raisi au kiongozi yeyote kuongoza nchi kwa matamko bali kwa kufuata katiba.​
>Maboresho ya haki za binadamu:
Kila binadamu atambuliwe utu wake, heshima, haki ya kuisha, haki ya malazi n.k;
  • Mfano, Kwa Tanzania wafungwa waliopo magerezani wanaishi kwa namna ambayo ni zaidi ya watumwa, ambapo katika magereza watu wamejaa mpaka sehemu za kulala hamna, Kazi wanazofanyishwa ni ngumu kupita kiasi, chakula hakiwatoshi, adhabu ya viboko wakati wa shughuli za kilimo n.k, Suala hili linatakiwa kutazamwa upya kikatiba na hivyo kuboreshwa.
  • Kwa Tanzania mahakama haina uhuru kamili katika maamuzi yake, Ndiyo maana rais anaweza kuiamuru mahakama ifute kesi kupitia kwa DPP hata kama kesi ina ushahidi.
  • Suala la haki za kisiasa linatakiwa pia kutazamwa upya, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanatekwa, kubambikwa kesi na wengine kukimbia nchi. Katiba mpya inaweza kutatua hili.
  • Suala la uthibiti wa Rushwa linatakiwa kuangaliwa upya na kutengeneza katiba mpya ili kila mtu apate haki pasina kuruhusu mianya ya rushwa.
Kwa ujumla wake, Mabadiliko au uhitaji wa katiba mpya siyo takwa la kisiasa kama ambavyo watu wanalichukulia bali ni hitaji la mwanadamu yeyote katika kuyakabili mabadiliko mbalimbali anayoyapitia.
Ifahamike wazi kuwa kiongozi au nchi kutekeleza wajibu wake wa raia haiwezi kuwa sababu ya kutotokea kwa mabadiliko ya katiba kwani katiba ndiyo itatoa mwongozo wa utekelezaji huo na kuchochea uwajibikaji.​

Pia suala la katiba mpya ni suala mtambuka, kwani kupitia mabadiliko ya katiba mpya ndipo utekelezaji wa majukumu na uboreshaji wa maisha ya kila siku ya mwanadamu vitafanywa kwa usahihi na weredi mkubwa.

Ni ukweli usiopingika kua, Kiongozi yeyote anayekwepa mabadiliko ya katiba pale inapohitajika anakua hana maono ya mbali kwani katiba mpya huhusisha mabadiliko ya kweli katika maendeleo ya mwanadamu na nchi kwa ujumla.
Mwisho ila si kwa umuhimu tukumbuke kuwa,

"Mabadiko ya Katiba au Katiba mpya ni hitaji la kila mtu katika kukabili mabadiliko ya kila siku."

Imeandaliwa na Wakale [ Jina La Kubuni ]
 
Upvote 2
Back
Top Bottom