Umuhimu wa Kiarabu kuwa lugha Rasmi Tanzania

NI SAWA

Kiarabu kifundishwe mashuleni

Kujua lugha nyingi ni faida na hazina kubwa kwa Taifa letu

Lugha zingine za muhimu kujua ni pamoja na kifaransa, kihispaniola na kichina.
 
Badala ya kupigania lugha ya Kabila lenu iwe rasmi Tanzania,we bado una akili za kitumwa mpaka Leo,jikomboe hata kifkra tu
 
Kwani hatuelewani?
Hayo yote yanafanyikaje?
Wambie wao watumie kiswahili kuwa lugha ya taifa.
 
Kwa sasa tujikite kwenye kuboresha UFUNDISHAJI wa lugha ya kiingereza maana tuliopita kwenye mfumo wa shule/vyuo vya umma humu nchini tunaaibika kwenye interview/makazini.

Ni aibu kwa Taifa letu!
 
Kiarabu tunapeleka wapi sasa? Looh acheni kuwa wafia dini hivo ,, Kingereza ni muhimu kuliko lugha yoyote na kinatumika sana
 
Taasisi kama Muslim University of Morogoro na Madrasa zitasaidia sana kutoa walimu wa lugha tajwa.
 
Yafuatayo ni Kiswahili si Kiarabu!

Maneno hapa juu ni Kiswahili, ukiwa Dar unaweza kuona mwenyewe kwenye sanamu ya askari. Naunga mkono ingekuwa vema kama angalau shule kadhaa zingefundisha pia Kiarabu kama lugha ya kigeni maana kwa kuelewa Kiswahili vema pamoja na historia yake kweli afadhali uweze kusoma Kiarabu. Maana maandiko yote ya Kiswahili kabla ya enzi ya ukoloni yalikuwa kwa herufi za Kiarabu. Pamoja na maneno haya mengi yaliyopokelewa kutoka huko.
Ukitaka kujua hapo juu inasema nini nenda hapo wikipedia ya Kiswahili
 
KIINGEREZA IKISHIKA NAFASI YA KWANZA INAYOZUNGUMZWA DUNIANI.
BASI LUGHA YA [HASHTAG]#KIARABU[/HASHTAG] INASHIKA NAFASI YA KWANZA ULIMWENGUNI.
 
Utaishia kuskia shukrani na sabuni
 

Lugha hii irasimishwe kwenye madrasa na misikitini kama kilatini kilivyo kwa wakatoliki.
 
Ni kweli mkuu, nilikuwa Cairo na niliweza kupata mahitaji yangu dukani kwa kuongea Kiswahili na wenyeji kuongea Kiarabu, maneno mengi yanaingiliana. Lakini si vibaya kuweka Kiarabu kama somo mashuleni kwa watakaopenda kama vile ilivyo Kifaransa.
Hoja zuri angalau kwa shule kadhaa pia chuoni. Maana si vizuri mtu anaweza kusoma Kiswahili hadi uzamili na uzamivu lakini hana habari kabisa kuhusu Kiarabu. Huwezi kuelewa Kiswahili kwa undani bila kujua angalau kidogo historia yake na hii ni kukutana kwa lugha za Kibantu na Kiarabu kwenye pwani la Afrika ya Mashariki. Kiswahili kiliandikwa tangu karne kadhaa, kabla ya mwaka 1900 kwa herufi za Kiarabu pekee. Kuna watu wangapi Tanzania wanaoweza kusoma urithi huu wa utamaduni? Nenda Ulaya, pale utapata watu wanaosoma Kiswahili pamoja na Kiarabu.
Naweka picha inayoonyesha matini ya Kiswahili (kwenye sanamu ya askari , mtaa wa Samora, Dar)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…