longokaka
Member
- Jul 17, 2021
- 6
- 54
Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia Shuleni .
Mfumo wa utoaji elimu ndio kitu pekee kitachopelekea elimu kupokelewa vizuri na wahusika katika mahala sahihi .
Jamii yetu ya Tanzania imetawaliwa na lugha ya Kiswahili na kwa upande wa pili ni kwamba Kiswahili kimeidhinishwa kuwa ni lugha ya taifa . kwaio ni kwamba ufanisi mkubwa sana wa kuelewa kwa watanzania umeegemea katika nguzo ya lugha ya kisahili .
Mfano: Mara nyingi sana walimu hutumia kingereza kufundishia huku bado wakiambatanisha na tafsiri za Kiswahili kitu ambacho kinaleta mzigo kwa wasomaji kwenye ukariri wa kitu kwa lugha mbili .
Faida za Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia :-
1.) Inaivuta elimu katika mazingira ya kinyumbani ni kiwa na maana katika mazingira ya kijamii zetu na kuondoa utabaka kati ya msomi na jamii inayomzunguka.
2.) Ina rahisisha Zaidi ujengaji picha juu ya elimu inayotolewa na kuchochea uelewa pia inaua ile dhana ya kua mtu akiongea tu ki-ingereza basi inaonekana kua ni mtaalamu na ni msomi pia .
3.) Inaongeza hamasa ya usomaji sio tu kwa wanafunzi hapana, ila hata kwa walioko nyumbani ambao wanapendelea kupata elimu Fulani juu ya kitu Fulani.
4.) Inatupa njia ya kuweza kujiendeleza wenyewe vizuri nikiwa na maana ata uandaaji wa mitaala wa elimu utawezekana kwa urahisi .
5.) Inachochea ukuaji na upanukaji wa lugha ya Kiswahili pamoja na ukuaji wa uchumi kwa kudhibiti gharama zitumikazo kwa uaandaaji wa mitaala kutoka nje.
Ushauri juu ya namna ya kufanya :-
Tanzania tayari ina wataalamu wakutosha . Nadhani jukumu ni la serikali kuangalia kwamba inawatumia vipi ili kuhakikisha hili jambo linakwenda kutekelezeka .
NB: Naomba ieleweke kwamba sikatai uwepo wa lugha ya ki-ingereza ,hapana, ila ki-ingereza kibaki kama somo ili kirahisishe mawasiliano ya kigeni .

Upvote
34