kiwatengu
Platinum Member
- Apr 6, 2012
- 18,585
- 16,780
Hello watanzania wenzangu, mimi nina mapendekezo ambayo ningependa wadau wa elimu tujaribu kuyaangalia na kuya pa umuhimu...kutokana na swala la elimu kuwa muhimu kwa vijana wa nchi yetu nina pendekeza kanda nyingine zitengwe ziwe kanda maalumu kielimu ili kuwakomboa na adui ujinga ambaye bado hajafutika kwa wengi sasa..ni ukweli kwamba bado kuna maeneo ambayo elimu bado ni duni kutokana na mwitkio kidogo sana wa wananchi na wanafunzi kwa ujumla..kuna maeneo ambayo bado wanaipa elimu kipaumbele cha mwisho, hii inatokana na shule kutokuwa na walimu na miundo mbinu muhimu inayohitajika kwa ajil ya elimu bora..Mfano Kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara inahitaji kipaumbele tofauti na kanda ya Kaskazini ambao walau kielimu wamepiga hatua..na kanda nyingine ambazo bado ni duni zipewe kipaumbele ili kuleta usawa. Huko wapewe walimu zaidi, miundo mbinu kama Maabara na Maktaba zijengwe zaidi..Kusini jamani They need help.