Umuhimu wa kuheshimu watu wengine

Umuhimu wa kuheshimu watu wengine

Mwamba 777

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
2,055
Reaction score
3,535
HEBU ANGALIA UMUHIMU WA KUHESHIMU WATU WENGINE KWENYE DUNIA HII

i. Kuzaliwa kwako kumefanywa na watu wengine.

ii. Jina lako umepewa na watu wengine.

iii. Umepata elimu kutoka kwa watu wengine.

iv. Kipato chako kwa namna fulani kinatoka kwa watu wengine.

v. Hata Heshima uliyonayo unapewa na watu wengine.

vi. Wa kwanza kukuogesha ni watu wengine.

vii. Wa mwisho kukuogesha pia watakuwa watu wengine.

viii. Mazishi yako yatasimamiwa na watu wengine.

ix. Utapelekwa kuzikwa na watu wengine.

x. Kila unachokimiliki kitarithiwa na watu wengine.

Sasa kwa nini unakuwa na kiburi,dharau na Majivuno dhidi ya watu wengine ? Pendaneni.

Kumbuka hakuna sehemu yoyote katika maisha yetu isiyohitajia watu wengine.

Ni matumaini yangu ujumbe huu utasomwa na watu wengine.
 
Back
Top Bottom