Umuhimu wa kujifunza saikolojia

Umuhimu wa kujifunza saikolojia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
HUWEZI hata kidogo kutenganisha maisha ya mwanadamu na elimu ya

saikolojia, elimu ambayo katika ulimwengu wa sasa wengi wanaisikia lakini

ni wachache wanaotambua umuhimu wake, achilia mbali maana ya neno lenyewe.


Injinia wa kwanza aliyeipa nguvu elimu hii ni mwanasaikolojia wa Kijerumani, Wilhelm Wundt ambaye alifungua maabara iliyokuwa ikifanya utafiti na kutibu watu kwa kisaikolojia, zoezi ambalo lilileta matokeo ya kushangaza ulimwenguni. Huo ulikuwa mwaka 1879.


Saikolojia ni ‘mtoto’ wa neno la Kigiriki lijulikanalo kama ‘psyche’ au akili na roho jina ambalo baadaye lilikuzwa na kufahamika kama Psychology, tafsiri ikiwa ni Elimu ya Nafsi na Ufahamu.


Katika nchi zilizoendelea, somo hili linapewa nafasi ya juu katika maisha ya binadamu kutokana na umuhimu wake. Wanasema wataalamu kuwa, kuishi bila kujua tabia za vitu na watu, ukuaji wake na kujifunza mabadiliko yake ni sawa na kutembea katika kamba ndogo ya maisha salama.


Saikolojia ni somo ambalo kila kukicha binadamu anatakiwa kufundishwa kwa vile hakuna anachoweza kukifanya kisiguse akili na nafsi yake. Inashauriwa kwamba ni lazima mtu ajifahamu mwenyewe, awafahamu wengine, mazingira anayoishi na mabadiliko yake.


Maswali ya msingi yenye kumuongoza binadamu vizuri katika maisha yake ni haya; Mimi ni nani, kwa nini niko hivi? Wale ni 80 akina nani, kwa nini wako vile na tunapaswa kuwa vipi baadaye, pamoja na kujiuliza kwa nini vitu vipo kama vilivyo.


Imebainika kwamba, mvutano wa nguvu za dunia na za binadamu huongezeka mara dufu kwa mtu ambaye hajui Saikolojia ya Maisha. Dunia kama sayari na mwanadamu kama kiumbe kila mmoja amekuwa

akitengeneza nguvu zake za kumuwezesha kuwepo, huku uzalishaji wa nguvu hizo kwa upande mmoja ukikinzana vikali na mwingine, hata hivyo madhara makubwa yamekuwa yakiwakuta binadamu ambao ndani yao kuna uhai.


Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kwamba, ufahamu wa nafsi na akili umebaki kuwa kinga muhimu ya mwanadamu katika ulimwengu huu ambao umekuwa ukibadilika mara kwa mara.


Hatari inayokuwepo kwa baadhi ya binadamu siku hizi hasa wa ulimwengu wa tatu, ni ukosefu wa elimu hii muhimu, jambo ambalo limewafanya watu wenyewe kwa wenyewe kuzalishiana nguvu za kuangamizana na kuiacha dunia ikishinda.


Inahuzunisha pia kufahamu kwamba, mbali na binadamu kushindana na mabadiliko ya ulimwengu na nguvu zake, wengi wao wamekuwa wakipambana na nguvu zao wenyewe ndani ya miili yao bila kujijua, kiasi cha kupoteza maisha.


Tafiti za wanasaikolojia zinaonesha kwamba, asilimia kubwa ya matatizo yanayomwangaisha binadamu yanatokana na yeye mwenyewe au jamaa zake, huku ushahidi ukionesha kuwa hata magonjwa ya kutisha

kama ya moyo, kansa, kisukari, vidonda ya tumbo na mengineyo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mawazo ya watu wenyewe.

WENGI kati ya watu wanaosumbuliwa na matatizo yanaoitwaya dunia ni wale wanaopambana na nguvu zao bila kujua. Kwa kutumia akili zao vibaya, hujitesa kwa kufikiri na kutafsiri vibaya matukio ya kila siku yanayotokea duniani.

Kama nilivyowahi kusema katika moja ya makala zangu nilizochapisha kwenye toleo la kitabu changu cha pili cha saikolojia ni kwamba hakuna kitu kibaya katika ulimwengu kwa asili, isipokuwa mawazo ya mtu mwenyewe.


Kwa mfano, tukizungumzia kufa ambapo watu wengi wanaamini kwamba ni jambo baya, kuna wengine wanaona ni zuri ndiyo maana wapo wanaojiua, na kama tukisema vita ni hatari, bado kuna watu wanafurahia

vita kwa vile si wote wanaowahurumia wafao vitani hata kama wataona maiti zao barabarani kwa wingi.

Kama nilivyosema, duniani kuna nguvu mbili, ambazo ni za watu wenyewe na za ulimwengu, hii ina maana

kuwa hata mawazo ya mwanadamu ni nguvu na mtu anaposumbukia kuwaza jambo fulani kwa undani kiasi cha kuumiza moyo wake anakuwa anashindana na nguvu zake mwenyewe.


Ifahamike kuwa kadiri mwanadamu anavyozidi kuongeza nguvu ya kufikiri, iwe kwa kukua kimwili, kusoma na kujifunza mambo mengi zaidi, kwa asili anakuwa anaongeza nguvu ambazo asipokuwa makini anaweza kufa akishindana nazo badala ya kuzitumia katika kumsaidia kimaisha.


Kwa mfano, watu kutoka kabila la Wabarabeigi wanaopatikana mkoani Manyara, nchini Tanzania wanaishi maisha ya kuwinda wanyama na kula mizizi ya porini, hawawezi kukaa wakifikiri jinsi ya kupata gari kwa kuwa kwao gari halina maana. Kwao maendeleo ni kuwinda na kuzaliana.


Kwa maana hiyo linapokuja suala la maisha magumu litatokana na ukame na wala si ukosefu wa mitaji au kazi. Hawa hawawazi magari kwa sababu hawajajifunza umuhimu wake, hawajui umuhimu wa kuwa na

zahanati, hospitali na wala bei ya mafuta haiwasumbui. Lakini kwa Wachaga waliozoea umeme wakikosa huduma hiyo kwao hilo litakuwa ni tatizo kubwa litakalowakosesha usingizi.


Vivyo hivyo, kwa watu waliozoea kutibiwa kwa sindano na vidonge, wakikosa tiba hizo itakuwa rahisi kwao kufa, kwa sababu akili zao zinatafsiri ukosefu huo kama tatizo kubwa kwao, lakini haiwi hivyo kwa

Wasukuma wanaoishi maporini kusikokuwa na hospitali za rufaa wala umeme.

Tafsiri ya hili ni nini? Ni fikra zitokanazo na kujua mambo na namna ya kuyawaza. Watu wengi siku hizi

wanajua utajiri, wanafahamu nini maana ya afya, wanaelewa umuhimu wa maendeleo lakini siyo wote wenye uwezo wa kukutana na changamoto hizo na kupata matokeo sahihi ya kile wanachokifahamu.


Kwenda hospitali kupimwa na kuambiwa kuwa una Kansa, Ukimwi, Kisukari, Pumu, TB na magonjwa kama hayo, siyo jambo linalowasaidia wengi kwa vile hawajui hatua ya kuelekea kwenye ujuzi huo wa mambo. Hapa ndipo elimu ya saikolojia inapohitajika ili iweze kumsaidia mtu anayejua mambo hayo namna ya kuyakabili, kuyaendeleza na kupata mafanikio.


Jambo la kusikitisha ni kwamba watu wengi wanaofahamu mambo hawafaidiki nayo na pale wanapojaribu kutumia ujuzi wao walioupata shuleni, wanajikuta wanaingia kwenye mapambano ya nguvu ya vile wanavyovifahamu.


Watu wengi leo hawalali usiku kucha wakipambana na yale waliyoyafahamu, utakuta mtu kakonda kwa sababu katambua mpenzi wake si mwaminifu, anakesha akilia bila kujua afanye nini kumaliza tatizo.


Mtu mwingine anakonda kwa sababu ni maskini, hana mtaji na ajabu nyingine kuna wanaosumbukia hata kasoro za maumbile yao ambazo wameumbwa nazo!
 
napenda sana somo hili la saikolojia na filosofia kwa kweli linakufumbua mambo mengi sana juu ya binadamu na namna ya kuishi.
laiti kama ningekuwa nishauri basi haya yawe ni masomo ya lazima kama development studies mavyuoni ilivyo ni lazima.
 
kuna mwandishi anaitwa Dale Carnigie, nimesoma vitabu vyake viwili How to Stop worrying and start living na How to win Friends and Influence, ni miongoni mwa vitabu vinavyosaidia mtu kuwafahamu watu,mazingira na jinsi ya kukabili changamoto zinazohusiana na mahusiano na watu na circumstances kadhaa.Nazidi kusoma mara kwa mara kama nisomavyo biblia
 

Kama nilivyowahi kusema katika moja ya makala zangu nilizochapisha kwenye toleo la kitabu changu cha pili cha saikolojia ni kwamba hakuna kitu kibaya katika ulimwengu kwa asili, isipokuwa mawazo ya mtu mwenyewe.

MziziMkavu wapi tutapata hicho kitabu hapa DAR na mikoani?
 


saikolojia inaweza ikamfanya mtu aonekane mchawi kwa wasiojua japo kuna ukweli ndaniyake saikolojia is the gun of life usipo ijua bunduki namna yakuitumia haiwezi kukusaidia ukijua kidogo inaweza kukusaidia au kukuangamiza mwenyewe ukijua matumizi yake .unajiamini na ina kusaidia cha msingi kaka mkuu uzidi kutupa somo usikate tamaa wala kutishika na comment za watu ukitishika utakua huja komaa katika kuitumikia saikolojia ulio nayo,,,100%
 
Last edited by a moderator:
saikolojia inaweza ikamfanya mtu aonekane mchawi kwa wasiojua japo kuna ukweli ndaniyake saikolojia is the gun of life usipo ijua bunduki namna yakuitumia haiwezi kukusaidia ukijua kidogo inaweza kukusaidia au kukuangamiza mwenyewe ukijua matumizi yake .unajiamini na ina kusaidia cha msingi kaka mkuu uzidi kutupa somo usikate tamaa wala kutishika na comment za watu ukitishika utakua huja komaa katika kuitumikia saikolojia ulio nayo,,,100%
Mkuu mimi ndio ninayotumia hiyo Saikolojia kuwatibu watu na kuwatatulia watu matatizo yao siku zote. Ni kweli ukijuwa saikolojia watu watakufikiri wewe ni mchawi kumbe unajuwa elimu ya kuwasoma moyoni mwao asante sana kwa ushauri wako.
 
kuna mwandishi anaitwa Dale Carnigie, nimesoma vitabu vyake viwili How to Stop worrying and start living na How to win Friends and Influence, ni miongoni mwa vitabu vinavyosaidia mtu kuwafahamu watu,mazingira na jinsi ya kukabili changamoto zinazohusiana na mahusiano na watu na circumstances kadhaa.Nazidi kusoma mara kwa mara kama nisomavyo biblia

Mkuu nakipataje hcho kitabu,,msaada wako tafadhali
 
Napenda sana hili somo!
MziziMkavu hongera sana kwa kuweka huu uzi hapa!
I hope nitakwenda na kurudi ili nikuulize maswali niliokosa majibu kuhusiana na hili somo!
...
But kwa kuanzia naomba utoe ufafanuzi ktk paragraph yako ya mwisho.... Hapooo uliposema kunawatu hawana raha dhidi ya maumbile yao!
Hapa kuna watu wengi wenye hilo tatizo. Mfano: wenye vipara/ualaza, wasio na shape, wafupi, na baadhi ya watu weusi, also kuna wenye vibamia na wengineo!
Naomba utoe maelezo ni vipi mtu anatakiwa kukabiana na jambo hilo.
 
Last edited by a moderator:
Napenda sana hili somo!
MziziMkavu hongera sana kwa kuweka huu uzi hapa!
I hope nitakwenda na kurudi ili nikuulize maswali niliokosa majibu kuhusiana na hili somo!
...
But kwa kuanzia naomba utoe ufafanuzi ktk paragraph yako ya mwisho.... Hapooo uliposema kunawatu hawana raha dhidi ya maumbile yao!
Hapa kuna watu wengi wenye hilo tatizo. Mfano: wenye vipara/ualaza, wasio na shape, wafupi, na baadhi ya watu weusi, also kuna wenye vibamia na wengineo!
Naomba utoe maelezo ni vipi mtu anatakiwa kukabiana na jambo hilo.
Kukabiliana na hali ya maumbile yako

inatakikana kwanza kujielewa wewe ni Binadamu umeumbwa na Mungu na Mungu hakufanya makosa katika vile

alivyokupa mwilini mwako. Ingawa Binadamu haridhiki na kile alichopewa na Muumba wake ndio utakuta mtu ana kipara

anatafuta dawa za kurudisha nywele.Utamkuta mwanamke anataka awe na kikalio kikubwa wengi wanataka wawe na

Maziwa makubwa, utamkuta mtu mwengine ana kibamia anataka awe na dushelele kubwa na kadhalika. Binadamu ni

kiumbe dhaifu sana ameumbwa na Mungu lakini anayo mapungufu yake binafsi kwa Mungu hakuna mapungufu wala

kasoro katika uumbaji wake kwa viumbe wake inatakikana utosheke na kile alicho kupa Muumba wako na Kuridhika ni

kitu muhimu kwa binadamu ninakuachia hapo kwaleo bibie Mashaxizo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom