Umuhimu wa Kumuunganisha Msajili wa Hati Miliki (Registrar of Titles) Kwenye Kesi ya Ardhi Ambayo Kiwanja Kimesajiliwa na Kina Hati

Umuhimu wa Kumuunganisha Msajili wa Hati Miliki (Registrar of Titles) Kwenye Kesi ya Ardhi Ambayo Kiwanja Kimesajiliwa na Kina Hati

Joined
Apr 26, 2022
Posts
83
Reaction score
128
Ukifungua kesi ya ardhi ambayo kiwanja kimesajiliwa au kina hati, unatakiwa kumshtaki pia na Msajili wa hati (Registrar of titles). Kushindwa kumuunganisha au kumshtaki Msajili kwenye kesi ambayo ardhi ina hati ni kumnyima haki ya kusikilizwa. Na hukumu yoyote itakayotolewa kwenye hiyo kesi bila Msajili kuunganishwa itakua ni batili.

Hii ni kwa mujibu wa maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenye kesi ya NESTORY MSOFFE & 5 OTHERS Vs THE REGISTERED TRUSTEES OF CATHOLIC ARCHDIOCESE OF ARUSHA CIVIL APPEAL NO. 254 OF 2019.

Je, hata kama sina ugomvi au malalamiko kuhusu usajili au mtu kupewa hati kwenye kiwanja chenye mgogoro bado kuna haja ya kumuunganisha na Msajili? Kesi hii haijajibu hilo swali, lakini kesi zingine zinasema utamuweka Msajili kama tu malalamiko yako yanahusu kusajiliwa au kupewa hati kwenye eneo lenye mgogoro.

Na ukimuweka Msajili (Registrar of title), hiyo inakua ni kesi dhidi ya Serikali (Government Suit), utatakiwa kumuongeza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General). Hivyo kwa kuwa ni kesi dhidi ya Serikali, utatakiwa kwanza uwape notice ya siku 90 kabla ya kufungua kesi ya ardhi ambayo mshtakiwa mmoja wapo ni taasisi ya Serikali.

FB_IMG_1721143893855.jpg
 
Back
Top Bottom