Umuhimu wa kunawa/kuosha mikono

Umuhimu wa kunawa/kuosha mikono

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mikono ni njia rahisi sana ya kusafirisha bacteria kwenda mdomoni. Mdomo na sehemu za siri ni lango la maadui kuingia mwilini (port of entry). Ngozi ikiyijeruhiwa pia inaweza kuwa lango lakini Leo nitazungumzia uhusiano wa mikopo na mdomo.

Fikiria unapokwenda haja hasa kwenye hizi ofisi zetu za umma na taasisi za serikali. Vingi kwanza unakuta mfumo wa maji chafu uliharibika siku nyingi seuse maji na sabuni ya kunawia unapomaliza.

Una rudi kwenye desk lako, una tumia kalamu, umehamisha bacteria kutoka chooni sasa wako kwenye kalamu. Wa pembeni yako au mteja anaazima kalamu atie sahihi kwenye karatasi, pasi kuelewa anabeba bacteria wale. Unakaribishwa andazi ofisini na kikombe cha chai. Kwa roho njema unawasafirisha bacteria tumboni na kwenye mwili kwa ujumla.

Fikiria unapopanda basi, unajua aliyeshika lile bomba alishika nini kabla? Au vile vyoo vyetu vya passport size kule kwetu Kwamtogole. Hujamliza kuna anaejusubiri nje aingie. Utakuwa na muda wa kunawa mikono kweli.

Tujijengee tabia ya kunawa mikono, kila mara hasa unapotoka chooni, kabla ya kula, baada ya kusalimiana na watu, unapoingia tu nyumbani au ofisini.

Kwa ofisini ni rahisi kuwa na kichupa cha alcohol gel pembeni ya meza yako.

Nyumbani kama huna bomba na sink la kunawia, tenga beseni dogo na ulitumie Mara tu ufikapo nyumbani.
Nitaweka picha yenye mwongozo wa kunawa mikoani. Kwa njia hii tutaepukana na magonjwa mengi hasa ya mlipuko.
 
Simu inayoongoza kwa uchafu
Mwanaume na mtu wake kitandani, wanashkashkana sehem za siri, vidole zamishwa ndan ya papuchi, Mara simu inaita, mavidole hayo yanakamata simu yakiwa mabichi toka kwenye papuchi,
Wakitoka sebulen na simu watoto hukimbilia simu ya baba na mama, mtoto kushika tu simu nakuanza kuinyonya simu[emoji2] [emoji2] [emoji1]
 
Simu inayoongoza kwa uchafu
Mwanaume na mtu wake kitandani, wanashkashkana sehem za siri, vidole zamishwa ndan ya papuchi, Mara simu inaita, mavidole hayo yanakamata simu yakiwa mabichi toka kwenye papuchi,
Wakitoka sebulen na simu watoto hukimbilia simu ya baba na mama, mtoto kushika tu simu nakuanza kuinyonya simu[emoji2] [emoji2] [emoji1]
Asante mkuu pia inatoka chooni unawahi simu isikatike, unanawa uanze kula simu inaita ni ya muhimu, unaipokea na unasahaukabisa kuwa uliishika ulipotoka chooni kabla ya kunawa
 
Back
Top Bottom