Umuhimu wa kunyonyesha mara baada ya kujifungua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Watoto wachanga wanapaswa kuanza kunyonyeshwa maziwa ya mama ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa ili maziwa yaanze kutoka mapema.

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) wanaeleza kuwa inashauriwa mara baada ya kujifungua mama na mtoto wagusane ngozi kwa ngozi ili kusaidia maziwa kutoka na kuongeza uhusiano kati ya mama na mtoto. Ni muhimu kwa mtoto kuwekwa kwenye titi ili aanze kunyonya maziwa ya mama.

Mama na mtoto wasitenganishwe, wawe pamoja muda wote, ila wanaweza kutenganishwa kwa ushauri wa daktari ikiwa kuna tatizo litakalomuathiri mtoto akiwa na mama yake mfano ugonjwa wa mtoto au mama.

Kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa kuna faida nyingi ikiwemo:

  • Kusaidia maziwa ya mama kuanza kutoka mapema na mtoto kupata maziwa ya mwanzo ya njano.
  • Kusaidia tumbo la uzazi kurudi katika hali yake ya awali na kupunguza kutoka damu nyingi baada ya kujifungua.
  • Kusaidia kumpa mtoto joto
  • Kujenga uhusiano wa kihisia na upendo kati ya mama na mtoto
  • Kusaidia kuchochea maziwa kutoka kwa wingi
Umuhimu wa maziwa ya njano kwa mtoto
Maziwa ya njano ni maziwa ya mwanzo, mazito yenye rangi ya njano ambayo hutoka siku chache za mwanzo baada ya kujifungua. Maziwa haya ni chakula kamili chenye virutubishi vingi, na pia yanatoa kinga maalum dhidi ya maradhi.

Aidha maziwa ya njano humsaidia mtoto kutoa kinyesi cha mwanzo chenye rangi ya kijani au nyeusi ambacho humfanya mtoto aumwe tumbo siku za mwanzo kama hatanyonya.

Virutubisho vilivyomo kwenye maziwa ya mama
Maji 87%
Wanga 7%
Mafuta 4%
Protin 1%
Vingine 1% (Vitamini, madini, kingamwili, vimeng'enya, Kiinitete)

Kunyonyesha kunampunguza hatari ya magonjwa kwa mtoto, mama

Mtoto anaponyonya inaweza kumsaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa yafuatayo:

Pumu
Unene kupita kiasi
Aina 1 ya kisukari
Ugonjwa mkali wa kupumua kwa chini
Maambukizi ya sikio
Ugonjwa wa kifo cha ghafla cha watoto wachanga (SIDS)
Maambukizi ya njia ya utumbo

Mama anaponyonyesha inaweza kupunguza hatari ya kupata magonjwa yafuatayo:
Shinikizo la damu
Aina ya 2 ya kisukari
Saratani ya ovari
Saratani ya matiti
 
Kuna post Jana iliwekwa ikidai mtoto apewe maji Mara baada ya kuzaliwa.... Iko Sawa hii ?
Mana hata mbuzi hafanyi vile
#Mnatuchanganya
 
Asante kwa taarifa mkuu tumekupata vyema

Somo zuri la lishe kwa kichanga
 
Kuna post Jana iliwekwa ikidai mtoto apewe maji Mara baada ya kuzaliwa.... Iko Sawa hii ?
Mana hata mbuzi hafanyi vile
#Mnatuchanganya
Hapana sio Sawa, Ndani ya miezi sita ya kwaza ya mtoto baada ya kuzaliwa ni vema akapewa maziwa ya mama pekee yake! Ama na dawa ama kwa ushauri wa daktari.
 
Uliona link ya hii case ya kumpa maji
 
Back
Top Bottom