Umuhimu wa kuoa Marekani ni zaidi ya kutaka kufuliwa

Prof Janabi wa JF

Senior Member
Joined
Jul 7, 2023
Posts
165
Reaction score
450
Tanzania mke anaonekana ndio mfuaji. Ila huku kufua ni jambo la kimashine zaidi. Na hata kama hamna mashine ya kufulia nyumbani viko vitu vya kufulia kwa gharama nafuu na hakuna maseke.

Mfano hizo ni mashine za kufulia na hakuna mtu hapo, unaweka hela unaweka nguo unafua ukimaliza kuna mashine za kukausha unasepa.

Hapo kuna kitundu cha kuweka sarafu ambazo wenyewe wanaita Quarters (dola sent 25). Hizo hapo juu ni mashine za kukausha nguo, unaweka quarters nne ili itimie dola 1, yaani kama haijatimia mashine haiwaki. Ila kimsingi zikitoka kufuliwa unaweza kuanika ndani zitakauka tu, ila kwa kufuata utaratibu unazikausha humo.


Basi bwana sabuni zenu za vipande kwa kweli hazina nafasi kwenye hizo mashine so kama hujabeba sabuni unatia quarters hapo kwenye mashine za sabuni unapata sabuni.

Mtoto wa kutoka kijijini baada ya kufika US anatamba tu. Kesho nitawaletea story za makahaba maana wananiganda kwelikweli kwenye one and two.
 
Hiyo mitambo hata hapa ipo ila gharama za umeme ziko juu sanaa, haileti maana kufulia nguo ya mtumba ya sh 5000 kwa gharama ya sh 3000........pia kuna nguo hiyo ya mtumba kuchanika kwasbb imechoka.
 
Hiyo mitambo hata hapa ipo ila gharama za umeme ziko juu sanaa, haileti maana kufulia nguo ya mtumba ya sh 5000 kwa gharama ya sh 3000........pia kuna nguo hiyo ya mtumba kuchanika kwasbb imechoka.
Ipo sehemu gani huko bongo na je, huduma ni self service kama huku USA (nilipo mimi 🙆🏾‍♂️) au unaacha nguo counter?.
 
Mimi hapa nilipo kuna mashine hadi ya kutawadha rinda. Mzungu maamaee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…