Umuhimu wa kupima afya zetu kabla ya kutumia dawa

Umuhimu wa kupima afya zetu kabla ya kutumia dawa

proton pump

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
6,814
Reaction score
10,104
Katika maisha yetu tunasumbuliwa na magonjwa ya aina mbalimbali ambapo inatulazimu kutafuta dawa za namna Fulani iwe za mitishamba au za hospitalini, suala hili wakati mwingine hutokana na kuwa na kipato kidogo au kukosa mda wa kufuatilia afya yako kwa wale wenye uwezo kifedha Jambo ambalo ni hatari kwa afya zetu.

Katika miili yetu dalili za ugonjwa huweza kutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine hii hutokana na Kinga alizo na mtu, hivyo ugonjwa sio wa kusoma nukuu au "notes" kimsingi Kama una uwezo Pima afya yako kabla kutumia dawa.

Tuchukulie kwa mfano magonjwa ya tumbo yanavyofanana fanana Kama vile vidonda vya tumbo, amoeba, minyoo, hata UTI huweza kusababisha maumivu ya tumbo hivyo ukimeza dawa Bila utaratibu huweza kusababisha vimelea vya magonjwa kuwa sugu, kudhuru afya yako.

Embu tuangalie faida za kupima afya zetu kabda kutumia dawa:

1. Kugundua tatizo linalokusumbua
2. Kutokudhuru afya yako kama kuumiza ogani kama vile ini na Figo.
3. Inatufanya uwe huru kisaikolojia baada kugundua tatizo.
4. Hupunguza gharama kwa kiasi Fulani endapo umegundua tatizo mapema.
5. Kujua aina gani ya tiba unayostahili.

Asante.
 
Back
Top Bottom