Trayvess Daniel
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 651
- 1,244
Wasalaam wanaJF,
Nikienda moja kwa moja kwenye mada, serikali iliyopo madarakani imekuwa na kawaida ya kudharau sana wananchi na kufanya wanachotaka.
1. Kodi zisizo na ulazima tena kwa vitisho na kejeli.
2. Matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Hii sio kwa wapinzani tu, kuna raia wa kawaida wengi sana wanakandamizwa na sheria kwa sababu ya kukosa watetezi.
3. Matumizi mabaya ya madaraka kunyanyasa wengine. Hii imekua kama ni aina ya maisha, kila mwenye cheo nchi hii moja kwa moja anaweza kutumia madaraka atakavyo na asifanywe chochote.
4. Na mengine mengi yanayoendelea nchini na bado yatazidi kukua na kukua kufanya maisha magumu kwa wanachi wenye vyama na wasio na vyama.
KUBWA KULIKO YOTE NI KWAMBA SERIKALI INATUMIA KODI ZETU WENYEWE KUTUNYANYASA, BILA KODI YA KUTOSHA SERIKALI YETU HAINA KITU.
Suluhisho la kutatua dharau za viongozi na maamuzi yenye maumivu makubwa kwa wanachi ni KATIBA MPYA, KATIBA YA WANANCHI, KATIBA YA WARIOBA.
kususia kunakuja na maumivu makali lakini matunda yake ni makubwa.
● Kuna jopo kubwa la vijana hawana ajira miaka na miaka
● Kuna jopo kubwa la vijana wamejiajiri lakini kodi zimekua kikwazo
● Sekta binafsi zinakosa uwezo wa kuajiri watu wengi
● Huduma za afya ni majengo na hakuna huduma za kueleweka
● Kuna jopo kubwa la watu wana kesi za kubambikiwa wamejaa mahamakani.
Nchi hii maisha ni magumu kwa walio wengi na huu ni mwanzo kama hatupo tayari kuilazimisha serikali kutusikiliza.
JE, TUNASUSIA KWA NAMNA GANI? nitakuja na uzi tofauti