MWANAHARAMU
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 4,041
- 10,699
Ustaharabu ni nini?Sijakataa wala kupinga madhara ya Dini katika jamii
Dini haikuleta hayo isipokuwa njia iliyotumika kusambaza Dini mbili hizi kubwa za Uislam na Ukristo ndiyo iliyohusisha Mauaji hasa ya kutumia Upanga, yaani usambazaji wa Dini kwa njia ya Upanga na umwagaji Damu
Kwa Dini zingine haya hayakuwahi kutokea kwa mfano Budhism, Hinduism na zingine zenye waumin mamilioni
Suala la Ustaarabu....NDIO, Dini ilikuja na Ustaarabu Afrika na kwa baadhi ya sehemu zilizokuwa na ustaarabu wa kale Dini ilibadikisha pia, kwa Mfano Mali, Ethiopia, Ghana na Zimbabwe. Mathalani Dini ya Ukristo ilikuja na Elimu ya kikoloni...ilimtaka mwanafunzi avae kaputula na shati jeupe, ilimfanya ajue kuoga kila mara, achane nywele na akimaliza kusoma aajiriwe na kuvaa suti na Tai
Hii ilienda mbali mpaka katika lifestyle ya Mwafrika kwa ujumla mpaka leo hii
Dini ya Uislam hali kadhalika na hii imegusa maeneo mengi zaidi
Mstaharabu ni nani?
Unasema haijaleta ila unakubali vipi ndugu wanapokuwa na Imani tofauti?
Nilichoona ni contradiction tu.