Habari wafugaji Leo tutajifunza juu ya utoaji wa iron injection kwa watoto wa nguruwe
π΄ UMUHIMU WA KUWAPA IRON INJECTION VITOTO VYA NGURUWE;
1. β
Kuzuia anemia (upungufu wa damu):
Nguruwe wachanga huzaliwa na kiwango kidogo cha chuma, hivyo bila iron injection wanaweza kuishiwa damu.
2. β
Kuongeza ukuaji na afya:
Chuma huongeza uwezo wa kubeba oksijeni kwenye damu, hivyo kusaidia ukuaji wa haraka na nguvu.
3. β
Kuimarisha kinga ya mwili:
Hupunguza hatari ya magonjwa kwa kuwa nguruwe anakuwa na afya bora.
4. β
Kuboresha ufanisi wa uzalishaji:
Nguruwe wenye afya hukua haraka na kufikia uzito wa soko mapema.
5. β
Kurekebisha upungufu wa chuma kwenye maziwa ya mama:
Maziwa ya mama nguruwe hayana kiwango cha kutosha cha chuma, hivyo sindano husaidia kujaza pengo hilo.
Muda Bora wa kutoa:
β‘οΈ Siku ya 3 baada ya kuzaliwa na kurudiwa Tena siku ya 21
Karibu sana tukuhudumie kwenye huduma ya matibabu,chanjo ,ushauri
Kwa mawasiliano
0674740836
0792263640