Theorist Mosses
JF-Expert Member
- Jul 16, 2022
- 345
- 253
(Pichani ni mwana anga Wa NASA)
Utangulizi
maendeleo, ni hatua inayochukua nafasi kwenye kuboresha jambo na kuhakikisha jambo linakuja kufanikiwa kupiga hatua moja kwenda nyengine na kuleta mabadiliko na matokeo chanya.
Sayansi ya anga, ni miongoni mwanguzo kuu za maendeleo ambazo nchi nyingi zimejikita ndani yake katika teknolojia zikiwa na dhumuni la kujihimarisha kwenye nyanja zote ikiwemo kwenye elimu, siasa, kilimo, biashara pamoja na kijeshi nk.
INTERNATIONAL SPACE STATION (ISS). ni kituo kikuu cha kimataifa cha anga za mbali ambacho kilirushwa kwenye anga mnamo mwaka 1998. lengo likiwa ni kukuza teknolojia ya maisha ya mwanadamu, ambayo inaukubwa sawa na viwanja viwili vya mipira wa miguu. Ipo takribani umbali wa 400km kutoka usawa wa bahari kuelekea juu na muundo wake ni mita za eneo 110, times 100, times 30 kitu ambacho ni kikubwa sana. Kinaenda speed ya 7.66km/s au 28,000km/h huku ikitumia nishati ya solar pannel (nishati ya jua) ndani ikiwa na maabara, pamoja na mashamba ya mimea ambapo binadamu wanafanyia chunguzi na tafiti za kisayansi.
Tunapo zungumzia sayansi ya anga tuna maanisha nini, sayansi ni ujuzi, maarifa makubwa sana yaliyo jikita zaidi kwenye utafiti na uchunguzi ambapo ndani yake yanaongozwa na nadharia kuleta ubunifu na ugunduzi ili kurahisisha maisha.
Taifa letu ni miongoni mwanchi ndogo zilizo nyuma sana kimaendeleo na uchumi mdogo katika nyanja nyingi ikiwemo kwenye sayansi na teknolojia. Leo nitaeleza tatizo linalo tufanya tushindwe kimaendeleo pia nitaeleza ni namna gani kwamba nini kianze kufanyika ili taifa letu liweze kujikwamua kiuchumi kwenye nyanja zote.
Sababu za msingi kuhusu kueleza juu ya umuhimu wa taifa letu kujikita kwenye sayansi ni Kwasababu sayansi ya anga imehakisi maisha yetu halisi tunayoishi ya kila siku. asimilia 75% ndani ya taifa letu tunaendesha maisha yetu kwakutegemea maendeleo ya sayansi na teknolojia.
lakini teknolojia tunayo itegemea siyo ya kwetu lakini ni bora zaidi kuweka malengo ambayo na sisi kama taifa huru tuka jihusisha kwenye sayansi itakayo tuokoa kwenye majanga ya kushuka kwa uchumi, kupunguza kupanda kwa gharama za maisha na kupunguza hongezeko la njaa.
Sayansi na teknolojia ndani ya taifa letu kunadhana ambazo zinachochea kukwamisha mikakati madhubuti katika teknolojia ambazo taifa letu limekuwa halitoi kipaumbele kuanzia kwenye Elimu, utafiti, chunguzi na nadharia. naomba tuzungumzie nadharia ambayo ndiyo nyenzo kuu ya msingi wa sayansi kwamba inaumuhimu gani katika mabadiliko na kimaendeleo ya taifa letu kwenye sayansi na teknolojia.
Nadharia.
Ni uelewa au ubunifu wa juu sana ambao unatumika kwenye teknolojia kuelezea, kufundishia, kutengenezea, kutafitia vitu vingi ambavyo vinakuja kujikita zaidi kwenye ugunduzi, elimu, kilimo, siasa na teknolojia.






(Pichani ni rocket inayoitwa starship imetengenezwa kwa nadharia na ubunifu)
Nadharia ndiyo nyenzo kuu kwenye sayansi na teknolojia iliyo hakisi maisha yetu halisi ambayo ni msingi wa maendeleo. Je, ni sababu zipi zinazo fanya taifa letu kushindwa kupiga hatua kwenye teknolojia ya sayansi na ipi ni njia bora ya kuinua teknolojia ndani ya taifa letu.
Vitu vinavyo changia kukwamisha maendeleo ya teknolojia ya sayansi hapa nchini.
• Taifa kuwa na wasomi wasio kuwa na vigezo kwenye sayansi na teknolojia. taifa kuwa na wasomi wasio kizi vigezo kuanzia walimu mpaka wanafunzi kwenye nafasi mbalimbali ni tatizo ambalo linachochea kujenga taifa lisilo kuwa na watu sahihi wenye ujuzi wa viwango vinavyo hitajika jambo ambalo linafanya taifa tushindwe kuendelea kwenye teknolojia.
• Taifa kuuwa vipaji vya vijana kwenye teknolojia. Ili ni pengo kubwa sana ambapo vijana wananyimwa haki zao za msingi wanapo jaribu kubuni au kugundua na kutengeneza chochote kinacho husiana na teknolojia ambapo kijana akitengeneza kitu basi mamlaka inamfungia kipaji chake asijihusishe na sayansi kitendo hiki kinachangia pia kupunguza kasi ya maendeleo katika taifa.
• Taifa kuwa na wasomi wasio wabunifu. Sisi kama taifa tunapo kuwa na wasomi ambao wasio na uwezo wa kugundua chochote au wakutengeneza hata vyombo vya usafiri ni tatizo kubwa linalo fanya taifa kushindwa kijukwamua kwenye teknolojia.
• Taifa kuwa na wasomi wengi wasio na malengo. Hili ni tatizo pale ambapo wasomi wanasoma tu bila kujiwekea malengo ambayo yangeweza kuchangia mchango mkubwa kwenye taifa kuhusu nyanja mbalimbali za maendeleo ili taifa liweze kujikwamua kiuchumi.
Vitu vitakavyo chochea maendeleo kwenye sayansi na teknolojia katika taifa letu
• Taifa kuwa na wataalam wenye malengo na ujuzi. Itasaidia sana kupiga hatua mbele kwenye suala zima la teknolojia ambapo taifa litanufaika kupitia kwa wataalam wenye malengo na maslahi bora kwaajiri ya kukuza uchumi wa taifa.
• Taifa kuhakikisha linaendeleza vipaji vya vijana. Nikitu ambacho kitasaidia sana kupunguza makundi mabaya ya vijana kama vile makundi ya kijambazi "panya road" kwamba taifa litakapo wasaidia vijana litakuza sayansi na teknolojia pia kwenye ajira.
• Taifa kuwa na wasomi wabunifu kwenye teknolojia. Itasaida taifa kupiga hatua kwenye sayansi na teknolojia ambapo wasomi watakuwa wakibuni vitu mbalimbali vitakavyo rahisisha maisha kwenye taifa itachochea kwenye uchumi.
• Taifa kuwa na kituo cha uchunguzi na tafiti za kisayansi. Hili pia ni nyenzo kuu itakayo saidia taifa kuendelea kiteknolojia na kupunguza gharama za maisha ambapo tutaweza kufanya safari ya anga za mbali na kutengeneza vitu vyetu wenyewe vikiwemo vyombo vya usafiri wa anga vitakavyo chochea uchumi na kukomesha kupanda kwa gharama za maisha ndani ya taifa.
Hitimisho
Tanzania kwenye sayansi na teknolojia inawezekana taifa bora zuri na imara hujengwa na watu wenyewe, lakini pia taifa bovu na baya hubomolewa na watu wenyewe.
(Pichani ni wana anga wa NASA wakiwa sambamba na kituo cha anga cha kimataifa ISS)
Upvote
18

