UTANGULIZI:
Haki ya kusahaulika ni haki ambayo inawezesha mtu kama kuna taarifa zake zimekusanywa na mkusanya taarifa yoyote, au mchakata taarifa, anaweza kwenda kuomba kwamba taarifa hizi mlizokuwa nazo kuhusu mimi sitaki muendelee kuwa nazo kwa sababu labda matumuzi yake yameisha au kwa namna moja au nyingine inaweza ikasababisha madhara kwake.
Katika zama hizi za kidigitali, taarifa binafsi za watu zipo katika majukwaa mengi, na mara nyingi hakuna uwezo wa kuzifuta kabisa taarifa hizi zisionekane na umma. Taarifa hizi zinashikiliwa na taasisi na makampuni binafsi n.k. Lakini si lazima taarifa hizo kubaki hivyo daima, na hapo ndio inaibuka haki ya kusahaulika ambayo mzizi wake unatokana na haki ya faragha.
Haki ya kusahaulika kwa mfano katika nchi za Ulaya imetolewa katika Sheria ya Ulinzi wa Data (GDPR), Sheria hii inawapa watu haki ya kufutwa / kusahaulika ili kulinda faragha ya watu binafsi kwa kuhakikisha kwamba wanaweza kudhibiti ni taarifa gani zinapatikana kuhusu wao mtandaoni. Haki hii inaruhusu watumiaji kuomba kufutwa kabisa kwenye mtandao kwa mambo ambayo wanaona hayana umuhimu tena au yamepitwa na wakati.
Kesi maarufu inayohusu haki ya kusahaulika ni kesi iliyoamliwa na Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya mwaka 2015 kwamba kulikuwa na haki ya kisheria ya faragha kwa raia wa Uhispania, Mario Costeja Gonzalez kuilazimisha kampuni ya Google Spain kufuta kumbukumbu za mtandaoni zinazohusu madeni yake ya zamani ambayo yalikuwa yameshalipwa.
Mahakama hiyo ilisema kwamba watu katika Umoja wa Ulaya wanaweza kuondoa mtandaoni taarifa binafsi ambazo zinaonekana kutokuwa na umuhimu tena.
Haki ya kusahaulika ni muhimu sana kwa kila binadamu japo asilimia kubwa ya watu hawafahamu umuhimu wa haki hii ya msingi inayoenda sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani taarifa zetu binafsi zinakusanywa na kuchakatwa na watu, makampuni na taasisi mbalimbali.
HAKI YA KUSAHAULIKA TANZANIA
Haki ya faragha ni pamoja na haki ya kusahaulika, au taarifa zako kulindwa, kwa mujibu wa sheria. Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetoa haki ya faragha na usalama wa mtu. Mara nyingi haki inayoongelewa ni haki ya faragha na ndio iliyotolewa na Katiba kwa Tanzania lakini haki hii inahusisha pia haki ya kusahaulika.
Tanzania kuna Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11, 2022 iliyoanza kutumika mwaka 2023, sheria hii imeanzisha Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo imezinduliwa rasmi mwaka 2024, ikiwa na majukumu mbalimbali yanayohusiana na ulinzi wa taarifa binafsi, ikiwemo jukumu la kupokea malalamiko yanayohusu uvunjifu na ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, pia Sheria hii imetoa haki za watu ambao taarifa zao zinakusanywa na kuchakatwa, namna ya kukusanya, kutumia na kutoa taarifa za mtu binafsi, na pia kulingana na Sheria hii watu wote wanaoshughulika na kukusanya na kuchakata taarifa za watu wametakiwa kujisajili kwenye Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Lakini sheria hii haijaongelea kuhusu haki ya kusahaulika, kwa maana hiyo nchini Tanzania hakuna haki ya kusahaulika kwani hakuna sheria inayotambua haki hiyo. Watu wengi wanatamani kusahaulika lakini hawajui wafanye nini, maeneo mengi watu hutoa taarifa zao ka nia njema lakini matumizi ya taarifa hizo huweza kufika mwisho, nini kinafuata?, Waliokusanya taarifa wanabaki nazo, zinatumika kufanyia nini?,
Tunapoamua kufunga akaunti zetu za Benki taarifa zetu tulizotumia kujiandikisha zinatumika vipi?, Vipi kuhusu tunapoamua kubadili namba za simu au kuhama mtandao wa simu, je taarifa zetu tulizotoa kufungua laini zinatumika kufanya nini? Hatufahamu!. Hapa ndipo uhitaji wa haki ya kusahaulika unapokuja.
UMUHUMU WA HAKI YA KUSAHAULIKA
Kila mtu katika maisha anapitia vipindi tofauti, na si kila tunalofanya leo tutajivunia baadaye na tunatamani kuendelea kutunza kumbukumbu, vitu tunavyovipenda / kuvichukia hubadilika. Akili nayo inaendelea kukomaa na kubadilika.
Hivyo basi, kuwa na uwezo wa kufuta taarifa zetu ambazo hazina umuhimu kunaimarisha usalama wetu na amani ya akili. Ni jambo linaloweza kuboresha afya ya akili kwa kiasi kikubwa, na kuruhusu watu kusonga mbele bila kuishi kwenye kumbukumbu ya makosa ya zamani au taarifa potofu zinazowahusu.
Pia haki ya kusahaulika inasaidia kulinda heshima na sifa ya mtu binafsi katika jamii. Makosa ya zamani au taarifa potofu zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa maisha ya mtu, ikiwemo kupoteza kazi, kudhalilishwa hadharani, au kuathirika katika mahusiano binafsi.
Pia, kwa wale ambao wamekuwa wahanga wa uhalifu wa mtandaoni kama vile udukuzi au unyanyasaji wa mtandaoni, haki ya kufutwa inatoa fursa ya kuondoa athari za matukio hayo. Hii inawapa nafasi ya kurejesha usalama wao wa kidigitali na kuanza upya kwa amani zaidi.
KITU CHA MUHIMU KUZINGATIA
Haki ya faragha ni miongoni mwa haki muhimu sana kuhusiana na utu wetu. Na haki ya kusahaulika ni miongoni mwa vitu vinavyoifanya haki ya faragha kuwa na maana zaidi. Yoyote anayechukua taarifa kwako anatakiwa akueleze atatumia hizo taarifa kwa ajili ya nini na akizitumia nje ya makubaliano yenu hakikisha kwamba unaenda kwenye mamlaka (Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi) husika ili faragha yako ilindwe, ili mamlaka zikusaidie kupata haki yako.
HITIMISHO
Haki ya Kufutwa ni haki msingi ya kibinadamu. Ingawa nyaraka za Umoja wa Mataifa kama Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR) haitaji moja kwa moja Haki ya Kufutwa / Kusahaulika, lakini inajenga kanuni msingi ya faragha ambayo Haki ya Kufutwa inajengwa juu yake.
Tanzania tutakayo ndani ya miaka 5, ni Tanzania yenye Sheria zinazotoa na kulinda ipasavyo haki ya kusahaulika, kuna haja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuifanyia maboresho Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ili kuongeza haki ya kusahaulika.

Upvote
4