SoC04 Umuhimu wa matumizi teknolojia ya vifaa vya kielektroniki kwenye chaguzi za viongozi Tanzania

SoC04 Umuhimu wa matumizi teknolojia ya vifaa vya kielektroniki kwenye chaguzi za viongozi Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

King mipawa

New Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
2
Reaction score
3
Ili kuendelea na kasi ya kuendana na ukuaji wa teknolojia na mifumo ya mitandao upo umuhimu mkubwa wa Tanzania kuingia kwenye utumiaji wa vifaa vya kisasa vya kuendeshea chaguzi mbalimbali za viongozi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Hii itasaidia kwenda sambamba na mabadiliko ya sasa ya uwezo wa wapigakura kuhakiki taarifa zao kwa njia ya mtandao ambayo yataenda kuidhinishwa kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura wa awamu ya mwaka huu wa 2024.

Mabadiliko hayo ni vema kwenda pamoja na utengenezaji wa mfumo rasmi wa mtandao utaomwezesha mpiga kupiga kura akiwa mahali popote (online votting)kwa kutumia simujanja na kompyuta.

Kutokana na ukweli kwamba si kila mwananchi anamiliki simujanja na kompyuta, serikali itaandaa vifaa vya kielektroniki (kompyuta)kwenye vituo vya kupigia kura vilivyoidhinishwa ili kuwawezesha wapiga kura wasio na uwezo wa kupiga kura mtandaoni kwa kutumia simujanja(online voters).

Orodha ya majina ya wagombea, picha na utambulisho wa vyama vyao vitaingizwa kwenye mfumo rasmi wa kupigia kura ambapo mpigakura ataweza kuona taarifa zao.

Kutakuwa na waongozaji wa vifaa vya kielektroniki kwenye vituo vya kupigia kura ili kuwawezesha wasioweza kupiga kura kwa njia ya mtandao.

Wapiga kura wote wataingizwa kwenye mfumo huo rasmi wa kupigia kura kulingana na taarifa zao zote zilizopo kwenye daftari la kudumu la wapigakura, ikiwemo na matumizi ya alama za vidole kwenye mfumo ili kuwezesha urahisi wa kumtambua mpigakura aliyejiandikisha.

CHANGAMOTO ZILIZOPO KWENYE MFUMO WA UPIGAJI KURA WA SASA.
✓Kuwepo kwa idadi ndogo ya wananchi wanaopiga kura Kipindi cha chaguzi.

-Katikahaguzi nyingi ambazo zimekuwa zikifanyika kumekuwa na muitikio mdogo sana kwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura kutokana na sababu kadha wa kadha.

-Hili limechagizwa sana na sababu ikiwemo;
{•} Majukumu ya kazi.
-Baadhi ya makundi makundi yamekuwa na ufinyu mkubwa wa nafasi ya kupiga kura kutokana na ukweli kwamba kumekuwa na ugumu wa kuvunja ratiba ya kazi hususani wafanyakazi wa kila siku (daily workers)ama deiwaka kama ilivyozoeleka kwa kiswahili cha mtaani.Hivyo basi wananchi wengi hujali zaidi maslahi ya kazi zao na kushindwa kujigawa ili kutekeleza jukumu la kiraia la kupiga kura.

-Kiujumla majukumu ya kazi yamebeba dhima kubwa sana inayowapa ugumu wananchi wengi kwenda kwenye vituo vya kupigia kura Kipindi cha chaguzi wakiamini zaidi kwenye maslahi ya kazi zao za kila siku hususani zile kazi zinazohusisha muda mrefu kwa siku.

-MIFANO YA MAKUNDI AMBAYO YAMEKUWA NA UFINYU WA NAFASI YA KUPIGA KURA;
•Wafanyabiashara ama wafanyakazi walioajiriwa kwenye biashara ambao muda mwingi anatakiwa kuwa sehemu ya biashara kutoka asubuhi hadi jioni.Hapa tunajumuisha na kundi la wajasiriamali wadogo ikiwemo mama nitilie, machinga na wajasiriamali wa magenge.

•Kundi la baadhi ya wakulima wadogo wadogo ambao mara nyingi hushinda shambani.Wakulima hawa imekuwa ni ngumu sana kwa baadhi yao kuvunja muda wa kazi zao ikitokea umeingiliana na siku za baadhi ya matukio ya kiserikali ikiwemo chaguzi.

•Kundi kubwa la vijana waliojiajiri wenyewe kwenye shughuli za bodaboda ambao kutwa nzima hushinda kwenye vituo vyao vya kazi.Ni ngumu kwa baadhi ya vijana wa bodaboda pia kuahirisha shughuli zao hata kwa nusu saa ili aweze kushiriki zoezi la upigaji kura.

•Madereva mabasi, malori na makondakta pia wana uwezekano mkubwa wa kukosa muda wa kupiga kura kura kama ilivyo kwa kundi la bodaboda na madereva bajaji.

•Kundi la wasafiri pia hususani safari za mbali lipo kwenye mlengo mkubwa wa kukosa nafasi ya kupiga kura pia.

{•} Uvivu na karaha ya kusubiri foleni ya kupiga kura.
-Hapa tunapata kundi jingine dogo la wapigakura ambao nao kutokana na uvivu na kuepuka usumbufu wa kusubiri foleni wakati wa kupiga kura.

MOJAWAPO YA FAIDA AMBAZO ZITAKUWEPO KUTOKANA NA MATUMIZI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI NI KAMA IFUATAVYO;
(•) Ongezeko la idadi ya wananchi wanaopiga kura na kama ilivyo sasa ambapo wananchi waliojiandikisha kupiga kura ni wengi sana ikilinganishwa na wale wanaojitokeza kupiga kura.Hapa kila mwananchi aliyejiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura atakuwa ana uhakika wa kupata nafasi ya kupiga kura akiwa mahali popote pale.

Bila kuwa na wasiwasi wa kuathiri shughuli za kila siku za mwananchi, bodaboda atakuwa ana uhakika wa kupiga kura akiwa ametulia kwenye maeneo yake ya kila siku.

Mama nitilie mgahawani atakuwa hana muda wa kuahirisha shughuli zake kwa muda mrefu kusubiri foleni ya kupiga kura, msukuma toroli vivyo hivyo, mfanyabiashara, mjasiriamali na makundi mengine yote ambayo kazi zao nyingi ni za kila siku na za masaa mengi kwa siku.

(•) Hii itaongeza ufanisi wa zoezi la upigaji kura kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa vya kuendeshea zoezi la uchaguzi ikiwemo uhesabuji kura.

(•) Mwananchi ataweza kupiga kura akiwa mahali popote pale pasipo kwenda kwenye vituo vya kupigia kura na kutoa nafasi kubwa kwa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye chaguzi.Kwa maana kwamba awe safarini,awe kazini,awe nje ya eneo lake la makazi kwa muda mfupi maadamu awe amejiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura na taarifa zake ziwe kikamilifu kwenye mfumo rasmi wa kupigia kura.

Mwisho kabisa, upo umuhimu wa kuendelea na msisitizo wa namna ya kuendelea na kuongeza kwa upanuzi wa matumizi ya teknolojia ya mtandao kwenye nyanja mbalimbali kutokana na ukweli kwamba dunia ya sasa ipo kwenye juhudi nyingi na uwekezaji mkubwa kwenye masuala ya teknolojia.Vizazi vijavyo vitakuwa kwenye mlengo mkubwa sana wa kuja kutumia teknolojia ambazo tutakuwa tumeziacha na zile ambazo wataanzisha kwa wakati wao.

Umuhimu wa teknolojia ni mzuri pale ambapo inaonekana kuleta urahisi wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiserikali na hata kiuchumi kama ambavyo tumekuwa tukiona juhudi mbalimbali za matumizi ya teknolojia hizi kwenye baadhi ya taasisi za kiserikali ikiwemo vyuo,mamlaka kama vile TRA, shirika la umeme (TANESCO) shirika la ndege (ATCL) shirika la mawasialiano (TCRA), taasisi za kifedha (Benki), mitandao ya mawasiliano ya simu na nyingine nyingi.

Hii ndiyo itakuwa Tanzania ya matumizi ya teknolojia tunayoitaka, teknolojia ya mtandao iwe ni chachu ya urahisi wa shughuli za mtanzania kwa ya kwamba ukuaji wa teknolojia ukawe na urahisishaji wa baadhi ya shughuli na matukio kama ya uchaguzi.
 
Upvote 3
Kutokana na ukweli kwamba si kila mwananchi anamiliki simujanja na kompyuta, serikali itaandaa vifaa vya kielektroniki (kompyuta)kwenye vituo vya kupigia kura vilivyoidhinishwa ili kuwawezesha wapiga kura
La msingi zaidi hilo, vituo viwe kisasa na sio kuhesabu makaratasi. Itasaidia sana vituo kuwa kielektroniki.

Japo upande wa online na popote kuna masuala ya kiusalama yatazingua, unaonaje tukiiga mifumo inakotumika huko je wao wanapiga na simu?? Au wanaenda vituo vua kielektroniki.?

} Uvivu na karaha ya kusubiri foleni ya kupiga kura.
-Hapa tunapata kundi jingine dogo la wapigakura ambao nao kutokana na uvivu na kuepuka usumbufu wa kusub
Mleta mada vipi kama hii inasaidia kuchuja watu walio siriazi na siasa na kuwaacha wazembe. Tutamuaminije mvivu kutuchagulia Rais sisi? Hahahahaah!
 
Back
Top Bottom